Posts

Showing posts from July, 2026

Mpango wa Marupurupu kwa Wazee wa Vijiji Kuimarisha Utawala wa Mashinani.

Image
Serikali ya Kitaifa imepongezwa kwa uamuzi wa kuanza kuwalipa wazee wa vijiji marupurupu ya kila mwezi, hatua inayolenga kuimarisha ushirikiano wao na machifu pamoja na vyombo vya usalama katika kutekeleza majukumu ya kiutawala na kudumisha usalama mashinani. Akizungumza Mombasa, Kamishina wa Kaunti hiyo, Mohamed Noor Hassan, amesema marupurupu hayo yatawasaidia wazee wa vijiji kukidhi mahitaji yao ya kimsingi huku yakitambua mchango wao mkubwa katika kuhudumia jamii. Amesema wazee wa vijiji ni kiungo muhimu kati ya wananchi na serikali, wakichangia kwa kiasi kikubwa katika ukusanyaji wa taarifa za kiusalama, utatuzi wa migogoro na kuimarisha utawala bora katika ngazi ya jamii.              Wakati huo huo, Kamishina Noor amewataka wazazi kuwa waangalifu na kuwafuatilia watoto wao wakati wa likizo ya shule ili kuwakinga dhidi ya ushawishi wa makundi ya uhalifu na vitendo vingine vinavyoweza kuhatarisha usalama wao.   Amesisi...

Serikali ya kaunti ya Mombasa kuajiri wauguzi 573 kufuatia mgomo unaondelea.

Image
                                  Kufuatia mgomo wa wauguzi ambao unaendelea nchini na kutatiza shughuli za utoaji huduma za afya Serikali ya kaunti ya Mombasa imetangaza zoezi la kuajiri wauguzi 573 kwa kandarasi ili kuhakikisha huduma za afya zinaendelea kutolewa bila kukatizwa kufuatia mgomo wa kitaifa uliotangazwa na Chama cha Wauguzi Kenya (KNUN). Akizungumza katika mkutano na wanahabari gavana wa kaunti hiyo Abdulswamad Shariff Nassir amewahakikishia wakazi kuwa hospitali na vituo vyote vya afya vya umma katika kaunti hiyo vitaendelea kutoa huduma licha ya mgomo unaoendelea. Akiwahakikishia wakaazi wa Mombasa kuwa hakutakuwa na usumbufu wowote wa huduma za afya katika Kaunt hiyo. Amesema jukumu kuu la serikali ya kaunti ni kulinda maisha ya wananchi na kuhakikisha huduma muhimu zinaendelea kutolewa wakati wote.                       ...

KAUNTI YA MOMBASA YAREJESHA MRADI WA "SKILLS MTAANI", ZAIDI YA TAASISI 400 ZA MAFUNZO ZASAJILIWA

Image
        Serikali ya Kaunti ya Mombasa imesajili zaidi ya taasisi 400 za mafunzo zitakazoshirikiana na kaunti hiyo katika utekelezaji wa mpango wa Elimu Scheme – Skills Mtaani, unaolenga kuwapa vijana ujuzi wa ufundi na kuwawezesha kujiajiri. Mpango huo unalenga kuunganisha maelfu ya vijana wanaotafuta ujuzi na taasisi zenye uwezo wa kutoa mafunzo ya vitendo yanayokidhi mahitaji ya soko la ajira. Kupitia mpango wa Skills Mtaani, vijana watanufaika na mafunzo katika fani mbalimbali ikiwemo utengenezaji wa mikate na keki, urembo na henna, useremala, ushonaji na ubunifu wa mavazi, mabomba, ufundi wa umeme, uchomeleaji vyuma, ufundi wa magari, teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT), pamoja na taaluma nyingine. Serikali ya kaunti imesema mpango huo ni uwekezaji katika kuwawezesha vijana kiuchumi, kuwapa fursa za kujitegemea na kuimarisha maendeleo ya Mombasa kwa kupeleka mafunzo karibu na jamii. Akizungumza wakati wa hafla hiyo Gavana wa Kaunti ya Mombasa, A...

WAZIRI JOHO ASITISHA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MADINI ZA KAMPUNI YA TATA CHEMICALS MAGADI LIMITED

Image
                Waziri wa Madini, Uchumi samati na Masuala ya Bahari, Hassan Ali Joho, ameagiza kusitishwa mara moja kwa shughuli zote za uchimbaji madini za kampuni ya Tata Chemicals Magadi Limited hadi pale itakapotekeleza kikamilifu matakwa ya Sheria ya Madini, kanuni zake na sheria nyingine zote zinazosimamia sekta ya madini nchini Kenya. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya miaka kadhaa ya mazungumzo kati ya Idara ya Serikali ya Madini na Tata Chemicals Magadi Limited kuhusu wajibu wake wa kisheria chini ya Sheria ya Madini, kifungu cha 306, Kanuni za Leseni na Vibali vya Madini za mwaka 2017, Kanuni za Ukusanyaji na Usimamizi wa Mrabaha wa Madini za mwaka 2024 pamoja na mifumo mingine ya kisheria inayohusika. Licha ya mazungumzo hayo, masuala kadhaa muhimu ya uzingatiaji wa sheria bado hayajatatuliwa. Miongoni mwao ni ukosefu wa mkakati wa wazi wa uongezaji thamani wa madini, madeni ya upatanisho na malipo ya mrabaha, upungufu katika...

Mwaguya Aongoza Katika Kura ya Maoni ya Useneta kaunti ya Mombasa.

Image
                  Mgombea wa kiti cha Useneta wa Mombasa, Hamisi Mwaguya, ameibuka kinara katika kura ya maoni iliyofanywa na Swiss Polls, akiongoza kwa asilimia 27.2 ya uungwaji mkono, sawa na kura 1,435. Mwaguya amemshinda kwa tofauti ya asilimia 2.7 mpinzani wake wa karibu, Seneta wa Mombasa Mohamed Faki, aliyepata asilimia 24.5, sawa na kura 1,294. Uongozi wa Mwaguya katika kura hiyo ya maoni unampa mwanzo mzuri katika mbio za Useneta wa Mombasa, huku akionekana kupata msukumo wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.                   Pia inamuweka katika nafasi ya kuimarisha zaidi uungwaji mkono wake huku kampeni zikitarajiwa kushika kasi. Mgeni Mboto Hassan ameshika nafasi ya tatu kwa asilimia 10.3, akifuatwa na Bernard William kwa asilimia 9.9 na Victor Abayo kwa asilimia 9.5. Utafiti huo ulihusisha sampuli ya watu 5,284, una kiwango cha makosa cha pamoja au p...

KENYA YAVUNJA REKODI YA DUNIA KWA UPANDAJI WA MIKOKO MOMBASA

Image
Kenya imevunja Rekodi ya Dunia ya Guinness ya kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu wanaopanda miti ya mikoko kwa wakati mmoja, katika zoezi lililofanyika Jomvu, Kaunti ya Mombasa. Jumla ya watu 4,196, wakiwemo maskauti, wanajamii na wahifadhi wa mazingira, walishiriki zoezi hilo. Kati yao, 4,124 walitimiza masharti ya Guinness World Records, na hivyo kuvuka kiwango cha awali cha washiriki 3,001. Mafanikio hayo yanaunga mkono juhudi za serikali za kupanda miti bilioni 15 ifikapo mwaka 2032, huku yakilenga pia kurejesha mifumo ya ikolojia ya pwani na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.            Zoezi hilo liliongozwa na Huduma ya Misitu Nchini (KFS), Chama cha Maskauti Kenya na M-PESA Foundation, kwa kushirikiana na jamii pamoja na wadau wengine wa mazingira. Tukio hilo limefanyika chini ya kaulimbiu “Mikoko yenye Afya kwa Uchumi Endelevu wa Buluu na Ustahimilivu wa Tabianchi,” likisisitiza umuhimu wa mikoko katika kulinda mazingira ya pwani, b...

SISI NI DOLA CUP: Ushindani Mkali Kutarajiwa Hatua ya 16 Bora.

Image
         Timu ya Mombasa Sports Club imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Wonderers katika mchezo wa Sisi Ni Dola Super Cup uliochezwa katika Uwanja wa Mombasa Sports Club. Sudi Morris alifungua ukurasa wa mabao dakika ya kwanza, kabla ya Alex Chamwoma kuongeza la pili dakika ya 30. Wonderers walipata bao la kufutia machozi dakika ya 88 kupitia Nassoro Hassan kwa mkwaju wa penalti.        Katika mchezo mwingine, Kombani Youth iliifunga Mtwapa All Stars 2-1 . Mtwapa walitangulia kupitia Ali Msomali dakika ya pili, kabla ya bao la kujifunga la Alfani Idi dakika ya 13 kusawazisha. Mwinyi Malandi aliifungia Kombani Youth bao la ushindi dakika ya 59. Nahodha wa Mombasa Sports Club, Madigi , amesema anatarajia ushindani mkubwa katika hatua ya 16 bora, akisema timu zimeonyesha viwango vya juu na anaamini kikosi chake kitafanya vizuri.           Kwa upande wake, kocha wa K...

Serikali ya kaunti ya Mombasa Yazindua Kozi Mpya Kuimarisha Uchumi wa Bahari na Ajira kwa Vijana

Image
                          Serikali ya Kaunti ya Mombasa imezindua kozi mpya za mafunzo ya ufundi katika chuo cha Ufundi cha Mtongwe kwa lengo la kuwapa vijana ujuzi wa vitendo utakaowawezesha kupata ajira katika sekta ya uchumi samawati na maeneo mengine yanayokua kwa kasi pamoja na  kituo cha kulelea watoto na maeneo ya michezo ili kuwasaidia wazazi vijana, hususan akina mama, kuendelea na masomo yao. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdullswamad Sheriff Nassir amesema serikali ya kaunti imejizatiti kuhakikisha mafunzo ya ufundi yanakuwa njia ya moja kwa moja kuelekea ajira kwa kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi pamoja na kupanua programu za ukuzaji wa ujuzi. Akisema kuwa vyuo vyote vya ufundi vinavyotaka kushirikiana na serikali ya kaunti vitakutana wiki hii katika eneo la Tononoka ili kuandaa mfumo wa kuwaandaa vijana kwa ajira kupitia programu za maendeleo ya ujuzi ka...

Pwani Innovation Week 2026 Kulenga Kuanzisha Biashara Mpya 37,000.

Image
                Pwani Innovation Week 2026 Yalenga Kuanzisha Biashara Mpya 37,000 na Kuwawezesha Vijana Milioni 2 Maandalizi ya Pwani Innovation Week 2026 yameanza rasmi huku waandalizi wakitangaza mpango kabambe wa kuanzisha biashara mpya 37,000 katika ukanda wa Pwani na kufungua nafasi za ajira kwa takriban vijana milioni mbili. Hafla hiyo, ambayo ni makala ya saba na pia wataadhimisha miaka kumi ya kituo Cha SwahiliPot Hub Foundation, kuanzia Oktoba 26 hadi 31 ikiwakutanisha wabunifu, wajasiriamali, wawekezaji na wadau kutoka Kenya na nchi mbalimbali ulimwenguni. Mwenyekiti wa Pwani Innovation Week, Kevit Desai, emsema tukio hilo limekuwa kichocheo muhimu cha ubunifu na ujasiriamali, likichangia kuanzishwa kwa zaidi ya biashara 4,000 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Akibainisha kuwa mwaka huu lengo ni kupanua mafanikio hayo kupitia ushauri wa kitaalamu, mafunzo, ujenzi wa mitandao na fursa za biashara kwa maelfu ya vijana. ...

Idara ya Polisi yapokea Vifaa vya Kisasa Kuimarisha Utekelezaji wa Sheria za Trafiki

Image
Shirika la Global Road Safety Partnership (GRSP), kupitia mpango wa Bloomberg Philanthropies Initiative for Global Road Safety (BIGRS), limekabidhi Huduma ya Kitaifa ya Polisi vifaa vya kisasa vya kuimarisha utekelezaji wa sheria dhidi ya uendeshaji wa magari chini ya ushawishi wa pombe na kupunguza ajali za mara Kwa mara barabarani. Hatua hiyo inalenga kuwajengea uwezo maafisa wa Polisi wa Trafiki na kuimarisha utekelezaji wa sheria dhidi ya vihatarishi vikuu vya ajali, huku ikichangia utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kuhusu usalama barabarani.                   Mratibu wa BIGRS, Vipul Patel, amesema matumizi ya vifaa hivyo yatawezesha utekelezaji wa sheria unaozingatia ushahidi, kubaini madereva wanaoendesha wakiwa wamelewa na kusaidia kuokoa maisha kupitia usalama bora barabarani. "Utekelezaji madhubuti wa sheria ni njia muhimu ya kupunguza ajali, vifo na majeraha barabarani. Makabidhiano haya ya ...

Kampeni Zapamba Moto Kuelekea Uchaguzi wa Chama cha Dock Workers Union (DWU)

Image
Huku ikiwa imesalia takriban mwezi mmoja Kwa uchaguzi wa chama Cha wafanyikazi wa Bandari(DWU) kampeni za kumtafuta katibu mkuu wa chama hicho zinaonekana kupamba moto. Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari (DWU), Abubakar Mohammed Abdullahi , ameanza rasmi kampeni zake kuelekea uchaguzi wa chama utakaofanyika Agosti 13. Hadi sasa yeye ndiye mgombea pekee aliyetangaza nia ya kuwania nafasi ya Katibu Mkuu, akilenga kumrithi Simon Sang. Katiba ya chama hicho DWU inaeleza kuwa anayewania nafasi ya Katibu Mkuu lazima asiwe mfanyakazi wa sasa wa mwajiri husika, na mfanyakazi yeyote anayetarajia kugombea analazimika kujiuzulu kwa kutoa notisi kwa mwajiri wake. Abubakar ameongeza kasi ya kampeni kwa kutembelea maeneo mbalimbali ya makazi ya wanachama akitafuta uungwaji mkono kabla ya uchaguzi huo.  Abubakar ni miongoni mwa viongozi wa chama waliowahi kufutwa kazi katika Mamlaka ya Bandari Nchini (KPA) pamoja na maafisa wengine wa chama kufuatia mgom...

Wakazi wa Lamu Wataka Kushirikishwa Katika Mradi wa Kituo cha Kusafisha Mafuta Cha Bilionea Dangote.

Image
Wakazi na viongozi wa Kaunti ya Lamu wameitaka Serikali kuhakikisha wanashirikishwa kikamilifu kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa kituo cha kusafisha mafuta chenye uwezo wa kusafisha mapipa 700,000 kwa siku, unaotarajiwa kujengwa na kampuni ya mfanyabiashara Aliko Dangote. Wakiongozwa na Sultan Omar Sharif, viongozi hao wamesema hawapingi mradi huo, bali wanataka Serikali iwe wazi na kuwahusisha wakazi wa eneo hilo katika kila hatua ya utekelezaji ili kuhakikisha wanapata manufaa ya moja kwa moja. Sultan Sharif amesisitiza kuwa ajira zinazotarajiwa kufunguliwa kupitia mradi huo, zinazokadiriwa kufikia zaidi ya nafasi 60,000 na zinapaswa kutanguliza wakazi wa Lamu.                            Aidha, ameitaka kampuni husika kutekeleza miradi ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) ikiwemo ujenzi wa shule, barabara na miundombinu mingine muhimu ili kuboresha maisha ya wananchi. Ameongeza kuwa mradi...

Kaunti ya Kilifi yazindua Kituo cha Uokozi kwa Manusura wa Dhuluma za Kijinsia

Image
Kaunti ya Kilifi imezindua rasmi na kukabidhi Kituo cha Uokozi kilichopo eneo la Fumbini, Wadi ya Kibarani, ambacho kitatoa hifadhi salama kwa manusura wa dhuluma za kijinsia (GBV) kutoka maeneo mbalimbali ya kaunti hiyo. Ujenzi wa kituo hicho umefadhiliwa na Children's Investment Fund Foundation (CIFF) na kutekelezwa na Shining Hope for Communities (SHOFCO) kwa ushirikiano na Serikali ya Kaunti ya Kilifi.                     Kituo hicho kitatoa huduma jumuishi ikiwemo ushauri nasaha, matibabu, malazi ya muda, mafunzo ya stadi za kujipatia kipato pamoja na maeneo ya watoto kucheza, ili kuwasaidia manusura kurejea katika maisha ya kawaida kwa heshima. Kwa muda mrefu, manusura wengi wa dhuluma za kijinsia wamekuwa wakikosa mahali salama pa kuishi baada ya kuripoti visa vyao, hali iliyowalazimu kurejea kwa watu waliowafanyia ukatili au kuendelea kuishi katika mazingira hatarishi. Kituo hiki kinatarajiwa kutatua ...

Zaidi ya familia 800 zaachwa bila makazi baada ya Nyumba 170 Kubomolewa Changamwe.

Image
Viongozi katika kaunti ya Mombasa wamekemea ubomoaji wa nyumba 170 katika makazi ya Kitaifa ya Changamwe National Housing Estate ulioacha zaidi ya familia 800 bila makazi. Viongozi hao wakiongozwa na Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi wakisema hatua hiyo ilifanyika licha ya kuwepo kwa amri ya mahakama kuzuia ubomozi. Viongozi hao wameonya kuwa uongozi wa ODM unaweza kutathmini upya uungaji mkono wake kwa serikali ya ushirikiano mpana (Broad-Based Government) kutokana na kile walichokitaja kuwa ni kupuuzwa kwa utawala wa sheria.                            Zaidi ya familia 800 zilivamiwa na msafara mkubwa wa maafisa wa polisi alfajiri ya leo wakati serikali ikianza utekelezaji wa mpango wa kubomoa nyumba hizo ili kupisha mradi wa ujenzi upya wa makazi hayo. Juhudi za viongozi wa eneo hilo kuwasihi polisi wawape wakazi muda wa kuokoa mali zao hazikufaulu, huku tingatinga likianza kubomoa nyumba hizo ...