Posts

Serikali Yaweka Zaidi ya Bilioni 721katika Ujenzi wa Nyumba za Bei Nafuu.

Image
       Serikali imewekeza fedha ya takriban Shilingi bilioni 731.5 katika mikataba ya ujenzi wa zaidi ya nyumba 280,000 zinazoendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali nchini kupitia Mpango wa Nyumba za Bei Nafuu. Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa kongamano la Kila mwaka la chama Cha wasanifu mijengo nchini AAK 2026 iliyofanyika Diani, Kaunti ya Kwale,  Kaimu Katibu wa Nyumba katika Idara ya Serikali ya Nyumba na Maendeleo ya Miji QS Cassius Kusienya, MBS,akiwakilisha na kusoma hotuba ya Katibu Charles Hinga amesema takwimu hizo zimetolewa katika taarifa ya hivi karibuni ya sekta na Principal Secretary Charles M. Hinga. Kwa mujibu wa hotuba hiyo, mpango huo kwa sasa unaendelea katika takriban kaunti 40, huku Serikali ikilenga kuufikisha katika kaunti zote nchini. Serikali pia imesema inalenga kuhakikisha kila eneo bunge kati ya 290 nchini linapata angalau nyumba 220, ikiwa sehemu ya mpango mpana wa kuongeza usambazaji wa nyumba za bei nafuu. Ku...

Wataalamu Wajadili Mustakabali wa Miji Katika Kongamano la chama Cha AAK Kwale.

Image
       Wataalamu na wadau wa sekta ya ujenzi wamekutana Diani, Kaunti ya Kwale, kwa Kongamano la Kila mwaka la chama Cha wasanifu mijengo nchinin (AAK), linalolenga kujadili namna ya kuifanya sekta ya mazingira yaliyojengwa kuwa himilivu dhidi ya changamoto za sasa na zijazo. Kongamano hilo linafanyika Diani kaunti ya Kwale, chini ya kaulimbiu “Shifting the Built Environment from Fragility to Resilience”. Kongamano hilo ni mkutano mkuu wa kila mwaka unaowaleta pamoja wataalamu na wadau kutoka sekta ya mazingira yaliyojengwa kujadili masuala yanayoathiri taaluma, sera pamoja na mustakabali wa miji na jamii. Akizungumza kwa niaba ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Idara ya Nyumba na maendeleo ya miji,Kaimu Katibu wa Nyumba katika Idara ya Serikali ya Nyumba na Maendeleo ya Miji QS Cassius Kusienya, MBS, amesema kaulimbiu ya mwaka huu inaakisi hali halisi inayokabili Kenya, huku miji ikikua kwa kasi kuliko mifumo inayohudumia wakazi.     Kw...

ODM Mombasa Yawaonya viongozi wa UDA kukoma Kuwashambulia Viongozi Wao.

Image
      Viongozi wa Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kaunti ya Mombasa wamewataka wenzao wa United Democratic Alliance (UDA) kukoma kuwashambulia  na kuwakosoa viongozi wa ODM, wakisema vyama hivyo ni washirika katika serikali jumuishi na Wala si maadui. Wakizungumza katika kaunti ya Mombasa,wakiongozwa na Mwenyekiti wao katika kaunti hiyo Mohamed Hamid Khamis amesema viongozi na wanachama wa ODM katika kaunti hiyo wamekuwa wakihamasisha wananchi kumuunga mkono Rais William Ruto na kueleza ajenda zake za maendeleo anapolenga kuwania muhula wa pili wa urais.     Khamis amehoji sababu ya baadhi ya viongozi wa UDA kulenga kuwashambulia viongozi wa ODM badala ya kushirikiana katika kuwasilisha ajenda ya serikali jumuishi. “Tunawauliza wenzetu wa UDA, sisi ni maadui wenu ama ni washirika wenu?” Khamis ameuliza. Amesema chama Cha  ODM Mombasa kitaendelea kuwahamasisha wanachama wake kumuunga mkono Rais Ruto, akisisitiza kuwa c...

Sarai Atetea Kauli ya Wafu Kupiga Kura, Awasihi Wakaazi wa Mombasa Kujitokeza Kupiga Kura.

Image
        Katibu Mkuu wa chama Cha United Democratic Alliance (UDA), Hassan Omar Sarai, ametetea kauli yake inayodaiwa kuwa na utata kuhusu wapiga kura waliokufa, akisema ilikuwa ni tamathali iliyolenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika usajili wa wapiga kura. Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Sarai amesema kauli zake zilikuwa na maana ya kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao. Sarai ameshutumu viongozi wa upinzani kwa kupotosha kauli zake na kuzitumia kama propaganda za kisiasa.     Amesema wapinzani wanapotosha kauli zake kwa sababu hawana ajenda ya maendeleo ya kuwaeleza wananchi na wanahofia kushindwa na chama tawala katika uchaguzi ujao. Sarai amesema matumizi ya lugha hiyo yalilenga kuhakikisha kila kura inahesabiwa katika uchaguzi ujao, huku akionyesha imani kuwa Rais William Ruto atashinda na kupata muhula wa pili. Hata hivyo katibu Mkuu huyo wa UDA ame...

Mzozo wa Umiliki wa Ardhi ya Shilingi Bilioni 1.5 Wazuka Samburu kaunti ya Kwale.

Image
         Mgogoro wa umiliki wa shamba lenye ukubwa wa ekari 3,100 na thamani ya Shilingi bilioni 1.5 umezuka eneo la Samburu, Kaunti ya Kwale, huku aliyekuwa mwakilishi wadi Saidi Mung’aro Nzuga na Rev. Fredrick Kanato Ndaikwa wakidai kuwa wao ndio wamiliki halali wa ardhi hiyo. Nzuga amesema yeye pamoja na Kanato walinunua shamba hilo kutoka kwa familia ya Mwachizi mwaka 2018, wakidai kuwa walifuata taratibu zote za kisheria na kufikia makubaliano rasmi na familia hiyo. Amesema wana nyaraka na barua mbalimbali zinazothibitisha kuwa walipata ardhi hiyo kihalali. Aidha, amefichua kuwa hati ya umiliki wa ardhi hiyo ilitolewa mwezi Aprili mwaka huu, baada kuhangaika kwa muda wa miaka Saba.           Hata hivyo, Nzuga anadai kuwa mhandisi Lung’azi Chai, ambaye analenga kuwania ugavana wa Kaunti ya Kwale, amejitokeza na kudai kuwa alinunua shamba hilo mwaka 2024 na kwamba ndiye mmiliki halali. Nzuga anadai kuwa Lung’az...

Familia Moja Samburu Yaililia Serikali Kulipwa Fidia ya Shamba Baada ya Miaka Miwili.

Image
    Familia ya Gari Kambe kutoka eneo la Samburu wadi ya Chengoni kaunti ya Kwale, imeitaka Serikali kuharakisha malipo ya fidia ya shamba lao lenye ukubwa wa ekari 98, ambalo walikubaliana kuliuza kwa Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa EPZ A Samburu. Kwa mujibu wa mwanafamilia, Ndaikwa Jumaa, familia hiyo ilifikia makubaliano na Serikali ya kuuza shamba hilo kwa bei ya shilingi 100,000 kwa kila ekari. Hata hivyo, Ndaikwa amesema licha ya makubaliano hayo, tayari miaka miwili imepita bila familia hiyo kupokea malipo yoyote. Familia hiyo sasa inaitaka Serikali kuingilia kati na kuhakikisha inalipwa fedha zake kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa. Ndaikwa amesema familia imetoa muda wa mwezi mmoja kwa Serikali kushughulikia suala hilo, ikionya kuwa iwapo haitalipwa ndani ya muda huo, italazimika kuchukua hatua zaidi ikiwemo kurejea katika shamba hilo na kuendelea na shughuli zao za ukulima. Familia hiyo ikiwa na Imani Serikali itaingilia kati kwa haraka ...

TotalEnergies Yazindua Kadi Mpya ya Malipo ya Kidijitali Nchini Kenya.

Image
       Wamiliki wa magari na wafanyabiashara nchini Kenya sasa wanaweza kufuatilia na kudhibiti matumizi ya mafuta kwa urahisi zaidi, kufuatia kuzinduliwa kwa mfumo mpya wa malipo wa kidijitali wa TotalEnergies Marketing Kenya. Kampuni hiyo imezindua Kadi Mpya ya TotalEnergies, inayolenga kuboresha usimamizi wa matumizi ya mafuta na kutoa njia salama na rahisi zaidi za kufanya malipo.       Kadi hiyo ni mageuzi ya bidhaa ambayo imekuwa katika soko la Kenya kwa zaidi ya miaka 25, baada ya kuanzishwa kama Bon Voyage Fuel Card, iliyokuwa kadi ya kwanza ya mafuta nchini Kenya na pia ya kwanza kutumia teknolojia ya chip. Kwa sasa, huduma hiyo imepanuliwa kuwa jukwaa kamili la kidijitali la malipo na huduma za usafiri kwa biashara, wasimamizi wa magari pamoja na madereva binafsi. Uzinduzi huo unafanyika wakati ambapo wafanyabiashara nchini wanazidi kutafuta njia bora za kufuatilia na kudhibiti matumizi ya mafuta kutokana na kuongezeka...