Sarai Atetea Kauli ya Wafu Kupiga Kura, Awasihi Wakaazi wa Mombasa Kujitokeza Kupiga Kura.

       

Katibu Mkuu wa chama Cha United Democratic Alliance (UDA), Hassan Omar Sarai, ametetea kauli yake inayodaiwa kuwa na utata kuhusu wapiga kura waliokufa, akisema ilikuwa ni tamathali iliyolenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika usajili wa wapiga kura.

Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Sarai amesema kauli zake zilikuwa na maana ya kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao.

Sarai ameshutumu viongozi wa upinzani kwa kupotosha kauli zake na kuzitumia kama propaganda za kisiasa.

   

Amesema wapinzani wanapotosha kauli zake kwa sababu hawana ajenda ya maendeleo ya kuwaeleza wananchi na wanahofia kushindwa na chama tawala katika uchaguzi ujao.

Sarai amesema matumizi ya lugha hiyo yalilenga kuhakikisha kila kura inahesabiwa katika uchaguzi ujao, huku akionyesha imani kuwa Rais William Ruto atashinda na kupata muhula wa pili.

Hata hivyo katibu Mkuu huyo wa UDA amepuuzilia mbali ukosoaji kutoka kwa baadhi ya viongozi wa upinzani.

Sarai amesema kuwasaidia wananchi walio katika mazingira magumu, wakiwemo wagonjwa, kufika katika vituo vya kupigia kura ni sehemu halali ya uhamasishaji wa wananchi kushiriki katika uchaguzi.

      

Aidha amesema kila mwananchi anapaswa kuwa huru kumpigia kura mgombea anayemtaka, huku akidai kuwa serikali jumuishi utaongeza idadi ya kura ambazo Rais Ruto anazo kwa sasa.

Sarai amesema uhamasishaji wa wapiga kura katika eneo la Pwani unalenga kuhakikisha wananchi wanatumia haki yao ya kikatiba na kuwa na ushawishi katika maamuzi ya kisiasa ya nchi.

Comments

Popular posts from this blog

Viongozi wa Kidini PPRL Waunga Mkono Agizo la wizara ya elimu la Ratiba ya Masomo Shuleni

Mbunge Feisal Bader Atuhumiwa Kuzuia Msambweni Talent Show Kufanyika Mvindeni Youth Centre.

Kaunti ya Wajir yaandaa Sherehe za Madaraka Day kwa mara ya kwanza tangu Kenya ipate Uhuru.