Posts

Showing posts from August, 2026

Serikali Yashinikizwa Kutunga Sheria kudhibiti swala la watu Kutoweka

Image
                                   Wanaharakati wa haki za binadamu na mashirika ya kiraia wametoa wito kwa Serikali na Bunge kutunga sheria inayotambua na kuifanya kuwa kosa la jinai vitendo vya watu kutoweka nchini Kenya. Wito huo umetolewa wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya uhamasishaji kuhusu watu wanaotoweka, huku wadau wakitaka hatua zaidi zichukuliwe kulinda waathiriwa na familia zao. Wangeshi Grace Kahuria kutoka IMLU, ambaye pia ni mwanachama wa Muungano wa Missing Voices Coalition na mratibu wa Police Reforms Working Group, amesema mamia ya visa vya watu waliopoteza maisha au kutoweka vimeripotiwa nchini kwa miaka kadhaa. Kahuria amesema visa 38 viliripotiwa mwaka 2019, 10 mwaka 2020, 36 mwaka 2021, 22 mwaka 2022, 10 mwaka 2023, zaidi ya 50 mwaka 2024 na visa sita mwaka 2025. Amesema hadi kufikia Agosti mwaka huu, visa 19 tayari vimeripotiwa.         ...

Kenya Kuimarisha Ushirikiano na ARSO, Yaahidi Ardhi ya Makao Makuu Nairobi.

Image
         Serikali ya Kenya imeahidi kutoa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu ya kudumu ya Shirika la Viwango la Afrika (ARSO) jijini Nairobi. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 32 wa ARSO unaofanyika Mombasa, Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha nafasi ya Kenya katika maendeleo ya mfumo wa viwango barani Afrika. Prof. Kindiki amesema Kenya inaona uwekezaji katika viwango kama msingi muhimu wa kukuza biashara, ushindani na maendeleo ya kiuchumi barani Afrika.             Amesema viwango vya pamoja vinaweza kupunguza gharama na ucheleweshaji wa biashara, akisisitiza umuhimu wa kaulimbiu ya mkutano huo ya “Kiwango Kimoja, Jaribio Moja, Cheti Kimoja, Kinachokubalika Kila Mahali.” Kwa mujibu wa Kindiki, mfumo huo utasaidia bidhaa kutoka nchi moja ya Afrika kukubalika katika masoko ya nchi nyingine bila kulazimika kufanyiwa vipimo na uthibitishaji wa mara...

KABRAS SUGAR YAMCHAPA KCB 15-5 NA KUTWAA UBINGWA WA SPORTPESA NATIONAL 7s CIRCUIT

Image
          Kabras Sugar wametawazwa mabingwa wapya wa Sportpesa National 7s Circuit  baada ya kuwalaza mabingwa watetezi KCB kwa alama 15-5 katika fainali iliyochezwa katika uwanja wa Mombasa Sports Club. KCB walichukua uongozi  dakika za mwisho za kipindi cha kwanza, baada ya Festus Shiasi kufunga try na kuwapa mabingwa hao watetezi uongozi wa 5-0 hadi kufikia mapumziko.      Hata hivyo, Kabras Sugar walianza kipindi cha lala salama kwa kasi, wakifunga tries tatu za haraka na kugeuza mchezo huo na hatimaye kushinda kwa alama 15-5. Daystar Falcons walimaliza katika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Menengai Oilers alama 21-5 huku  Uganda Emerging 7s wakimaliza katika nafasi ya tano baada ya kuifunga Nondescripts 19-14. Katika fainali ya Division Two, Zetech Oaks walitwaa ubingwa baada ya kuifunga Stallions Rugby kwa alama 33-7.        Kocha msaidizi wa Kabras Sugar, Ntabeni Dukis...

Sportpesa National 7s Circuit:KCB yatinga robo Fainali Kwa kishindo.

Image
                   Makala ya 36 ya mchezo wa Raga ya wachezaji saba Kila upande SportPesa National 7s Circuit, yanaendelea katika uwanja wa Mombasa Sports Club katika kaunti ya Mombasa huku Bingwa mtetezi KCB akianza mashindano hayo Kwa kishindo wakiongoza kundi B bila kupoteza mchezo. KCB ilianza kampeni kwa ushindi wa alama 22-5 dhidi ya Kisumu RFC, kabla ya kuishinda Uganda Emerging 7s kwa alama 12-7 katika mchezo wa pili. Katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi, KCB iliibuka na ushindi wa alama 29-10 dhidi ya KU Black Blad, na hivyo kufuzu kwa robo fainali itakayochezwa Jumapili.               Kabras Sugar walimaliza katika nafasi ya pili baada ya pia kutokupoteza mchezo. Waliifunga wenyeji Mombasa Sports Club Rugby kwa 43-0, kisha wakashinda Nondescripts RFC kwa 12-0. Hata hivyo, walilazimishwa sare ya 17-17 na Kenya Harlequins katika mchezo wao wa mwisho. NYS S...

Viongozi wa Kidini PPRL Waunga Mkono Agizo la wizara ya elimu la Ratiba ya Masomo Shuleni

Image
          Viongozi wa kidini wa Pwani Patriotic Religious Leaders (PPRL) wakiongozwa na Mwenyekiti wao Sheikh Abu Qatada, wameunga mkono na kupongeza agizo la Waziri wa Elimu Julius Migosi Ogamba kuhusu kufuata muda rasmi wa masomo shuleni. Kwa mujibu wa agizo hilo, masomo yanafaa kuanza saa mbili asubuhi na kutamatika saa tisa na nusu alasiri. Sheikh Abu Qatada amesema viongozi wa kidini na wazazi wamekuwa na wasiwasi kuhusu mzigo mkubwa wanaobebeshwa wanafunzi kwa kulazimika kuondoka nyumbani mapema alfajiri na kurejea jioni.          Amesema muda mwingi ambao wanafunzi hutumia shuleni umekuwa ukiwanyima fursa ya kukaa na wazazi wao, huku walimu wa madrasa pia wakikosa muda wa kutosha kuwafundisha elimu ya dini ya Kiislamu na maadili mema. Amesema ni muhimu watoto kupata elimu ya shule pamoja na elimu ya dini, akisisitiza kuwa hata kama mtoto atafanikiwa kuwa kiongozi au kufanikiwa kimaisha, bila kuwa na maadili...

MOMBASA MEGA MARATHON: KITUNDU NA CHERUIYOT WASHINDA MBIO ZA KILOMITA 42.

Image
                            Mwanariadha Little Nick Kitundu ameibuka mshindi wa mbio za kilomita 42 katika Mombasa Mega Marathon, baada ya kutumia muda wa saa 2:16:02. Kitundu alifuatwa na Gabriel Kahora, aliyemaliza katika nafasi ya pili kwa muda wa  saa 2:18:39, huku Theophilus Kipsang akimaliza wa tatu kwa muda wa saa 2:18:54. Kwa upande wa wanawake katika mbio za kilomita 42, Betty Cheruiyot alitwaa ushindi kwa muda wa saa  2:36:09. Akifuatwa na Lucy Chelele, aliyemaliza wa pili kwa muda wa saa  2:40:59, huku Anastacia Jepkoech akishika nafasi ya tatu kwa muda wa saa 2:42:27. Katika mbio za kilomita 21 upande wa wanaume, Justus Muasya alishinda kwa muda was aa 1:00:52, akifuatiwa na Elisha Kipsoi aliyemaliza wa pili kwa muda wa saa 1:02:55 nae Tom Mwendwa Mutie akishika nafasi ya tatu kwa muda wa 1:05:57. Akizungumza baada ya ushindi wake, Little Nick Kitundu amesema mbio hizo hazikuwa rahisi kutoka...

Starehe Bikeathon Yawasili katika kaunti ya Mombasa Baada ya Safari ya Kilomita 1,100.

Image
  Mbio za baiskeli za timu ya Starehe Boys Centre zimewasili salama katika kaunti ya Mombasa baada ya safari ndefu ya zaidi ya kilomita 1,100 iliyochukua takriban wiki mbili. Safari hiyo ilipitia maeneo mbalimbali ya nchi, ikiwemo Bonde la Ufa, Nairobi, maeneo ya ukambani  na milima ya Taita Taveta, kabla ya kufikia jiji la Mombasa. Waendesha baiskeli hao walipokelewa kwa shangwe na wafadhili wakuu wakiongozwa na Safaricom, St. John’s Ambulance na Vivo Energy. Tukio hilo linalojulikana kama Dr. Geoffrey Griffins Memorial Charity Bikeathon 2026, lilianza tarehe 3 Agosti mjini Busia kwa lengo la kukusanya zaidi ya shilingi milioni 10 zitakazotumika kusaidia wanafunzi wa Starehe Boys’ na Starehe Girls’ schools. Kiongozi wa kiufundi wa timu hiyo, Ian Hisho, amesema tayari wamefanikiwa kukusanya asilimia 10 ya lengo lao la shilingi milioni 10. Akisema wana matumaini ya kufikia lengo hilo kabla ya uzinduzi rasmi wa mpango huo mwishoni mwa mwezi huu.         ...

Gavana Abdulswamad Awataka Vijana Kukataa Siasa za Chuki na Ubaguzi.

Image
            Gavana wa Kaunti ya Mombasa, Abdulswamad Shariff Nassir, amewataka vijana kuachana na wanasiasa wanaoendeleza siasa za chuki na ukabila kuwagawa wananchi. Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Vijana Duniani, Gavana Abdulswamad amesema vijana wanapaswa kusikiliza sera za kila mwanasiasa na kutathmini namna anavyolenga kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa Mombasa.            Abdulswamad akiwataka vijana kuacha kufuata wanasiasa wasio na ajenda wala maono ya kubadilisha maisha yao, akisisitiza umuhimu wa kufanya maamuzi kwa kuzingatia sera na mipango ya maendeleo. Gavana amesema ukosefu wa ajira ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazowakabili vijana nchini, na serikali ya kaunti ya Mombasa imeweka mikakati mbalimbali ya kuwawezesha vijana kujikimu kimaisha.               Aidha, amewataka vijana kuwa na nidhamu na kujituma katika ...

MOMBASA MEGA MARATHON YAZINDULIWA, ZAIDI YA WASHIRIKI 1,000 WATHIBITISHA USHIRIKI WAO.

Image
                                     Mashindano ya Mombasa Mega Marathon yanatarajiwa kufanyika Jumapili, Agosti 16, baada ya kuidhinishwa na Shirikisho la Riadha nchini. Makamu wa Kwanza wa Rais wa shirikisho hilo, Paul Mutwii, amezindua mashindano hayo jijini Mombasa Jumatatu, akimwakilisha Rais wa shirikisho hilo Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei. Mutwii amesema wamefurahishwa na kurejea kwa mashindano makubwa ya Marathon Mombasa, baada ya kutokuwepo kwa miaka kadhaa.                                   Amesema Rais wa huyo amesaini kibali cha mashindano hayo, huku waandaaji wakitarajiwa kukabidhiwa kibali hicho wakati wa uzinduzi. Mashindano hayo yatakuwa na mbio za kilomita 42, kilomita 21, kilomita 10 na kilomita 5. Balozi wa Mombasa Mega Marathon, Omar Said, amesema zaidi ya washiriki 1,000 tayari ...

Wakazi wa Lamu Wataka Asilimia 70 ya Ajira Katika Mradi wa Kusafisha Mafuta wa Dangote.

Image
         Wakazi wa kaunti Lamu wameitaka Serikali kuhakikisha jamii inashirikishwa kikamilifu katika kila hatua ya utekelezaji wa mradi wa kusafisha mafuta, wakisisitiza kuwa ushirikishwaji huo ndio utakaowezesha wananchi kunufaika na mradi huo. Wakizingumza na waandishi wa habari wakiongozwa na Sultan Omar Sharif amesema wakaazi wameupokea na kuukaribisha mradi huo, ila wanataka kushirikishwa kwa asilimia 100 kuanzia hatua za upangaji hadi utekelezaji. Amesema vijana wa eneo hilo wanahitaji kupewa kipaumbele katika ajira, akitaka asilimia 70 ya nafasi za kazi zitakazozalishwa na mradi huo zitolewe kwa wenyeji pamoja na kupewa mafunzo ya kuwajengea uwezo. Aidha, ametaka asilimia mbili ya faida ya mradi irejeshwe kwa jamii kupitia mfuko wa maendeleo utakaosaidia kuboresha huduma mbalimbali na miundo mbinu.  Kwa upande wake, Bado Somo amesema makubaliano kuhusu manufaa ya mradi yanapaswa kuwekwa wazi na kuandikwa rasmi badala ya kutolewa katika ma...