KABRAS SUGAR YAMCHAPA KCB 15-5 NA KUTWAA UBINGWA WA SPORTPESA NATIONAL 7s CIRCUIT
Kabras Sugar wametawazwa mabingwa wapya wa Sportpesa National 7s Circuit baada ya kuwalaza mabingwa watetezi KCB kwa alama 15-5 katika fainali iliyochezwa katika uwanja wa Mombasa Sports Club.
KCB walichukua uongozi dakika za mwisho za kipindi cha kwanza, baada ya Festus Shiasi kufunga try na kuwapa mabingwa hao watetezi uongozi wa 5-0 hadi kufikia mapumziko.
Hata hivyo, Kabras Sugar walianza kipindi cha lala salama kwa kasi, wakifunga tries tatu za haraka na kugeuza mchezo huo na hatimaye kushinda kwa alama 15-5.
Daystar Falcons walimaliza katika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Menengai Oilers alama 21-5 huku
Uganda Emerging 7s wakimaliza katika nafasi ya tano baada ya kuifunga Nondescripts 19-14.
Katika fainali ya Division Two, Zetech Oaks walitwaa ubingwa baada ya kuifunga Stallions Rugby kwa alama 33-7.
Kocha msaidizi wa Kabras Sugar, Ntabeni Dukisa, amesema ushindi wao dhidi ya KCB katika mashindano ya hayo umewapa afueni baada ya timu hiyo kupata matokeo mabaya katika Kabeberi 7s.
Dukisa amesema Kabras iliingia katika mashindano ya Mombasa ikiwa chini ya presha kubwa, hali iliyowalazimu wachezaji kujituma zaidi ili kurejea katika hali yao ya ushindani.
Kwa upande wake, kocha mkuu wa KCB, Andrew Amonde, ameipongeza Kabras Sugar kwa kutwaa ubingwa wa Driftwood 7s, huku akisema kichapo hicho ni somo muhimu kwa timu yake kuelekea mashindano yajayo ya Embu 7s.
Amonde amesema KCB itatumia matokeo hayo kujipanga upya na kurejea ikiwa na nguvu zaidi katika mashindano ya Embu 7s.
Afisa wa mahusiano ya umma,mauzo na matangazo Mercy Kagui amesema mashindano hayo yamekamilika kwa mafanikio, huku akiwapongeza mashabiki na washiriki kwa kujitokeza kwa wingi.Akiwapongeza Kabras Sugar kwa kutwaa ubingwa.
Kagui amesema SportPesa imeongeza mgao wake wa udhamini kutoka shilingi milioni 14 hadi shilingi milioni 35, hatua inayolenga kuendeleza na kukuza michezo nchini.
Akisisitiza kuwa SportPesa haiungi mkono mchezo wa raga pekee, bali pia inawekeza katika michezo mbalimbali kama njia ya kuwawezesha vijana.
Aidha, amesema mashindano hayo yametoa fursa kwa vijana kuonyesha vipaji vyao, kujitangaza na kupata nafasi ya kugunduliwa na wachambuzi na wadau wa michezo, jambo linaloweza kuwasaidia kuendeleza vipaji vyao na kufikia viwango vya juu zaidi.
Comments
Post a Comment