Posts

Showing posts from May, 2026

Kaunti ya Wajir yaandaa Sherehe za Madaraka Day kwa mara ya kwanza tangu Kenya ipate Uhuru.

Image
  Kaunti ya Wajir imeandika historia kwa kuandaa sherehe za 63 za Madaraka Day kwa mara ya kwanza tangu Kenya ipate uhuru. Serikali imesema hatua hiyo inaonyesha dhamira ya kuhakikisha maendeleo na shughuli za kitaifa zinafikia maeneo yote ya nchi huku zikikuza umoja, usawa na mshikamano wa kitaifa. Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea maadhimisho hayo, Msemaji wa Serikali, Isaac Mwaura , amesema kuwa tukio hilo linaonyesha dhamira ya serikali katika kukuza ushirikishwaji, usawa na mshikamano wa kitaifa. Alibainisha kuwa licha ya changamoto za uchumi wa dunia, ikiwemo athari za mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati, uchumi wa Kenya umeendelea kuwa thabiti na hivyo kuwezesha serikali kuendelea kuwekeza katika maendeleo na umoja wa kitaifa.                    Maandalizi ya sherehe hizo yameleta mabadiliko makubwa katika mji wa Wajir, ikiwemo ujenzi wa uwanja wa kisasa wenye uwezo wa kuhudumia zaidi ya watu 10,000, ubo...

Wadau wasukuma mwani kutangazwa kama zao la biashara

Image
  NA SHOKA JUMA KIBUNI KWALE. Baadhi ya wadau wanaitaka serikali ya kitaifa kulitambua rasmi zao la mwani kama zao la biashara ili kufungua kikamilifu uwezo wake wa kiuchumi kwa jamii za pwani. Kulingana na Alfred Rono, Mratibu wa Mradi wa Mwani kutoka shirika la Plan International, mwani kwa sasa umeorodheshwa na kushughulikiwa kama samaki, licha ya kuwa ni mmea wa baharini wenye tabia na uzalishaji tofauti kabisa. Alisema kuwa kuiweka upya hadhi ya mwani kama zao la biashara kutawafanya wakulima na wajasiriamali wa pwani kunufaika kwa kiwango sawa cha usaidizi wa sera na uwekezaji kama ilivyo kwa mazao ya kawaida kama kahawa, chai na miwa. “Mwani si samaki; ni mmea wa baharini wenye uwezo wa kubadilisha maisha, hasa katika ukanda wa Pwani. Lakini kwa sababu hautambuliwi rasmi kama zao, wakulima hukosa fursa za usaidizi na miundombinu ya masoko,” alisema. Alitoa wito kwa serikali kupitia sera zake za kilimo na kulijumuisha zao la mwani katika orodha ya mazao ya biashara yaliyopang...

Viongozi kutoka kaunti ya Mombasa wajitokeza kumtetea Hassan Omar Sarai.

Image
Baadhi ya viongozi na wakazi wa Kaunti ya Mombasa wanaendelea kujitokeza kumtetea Katibu Mkuu wa Chama cha UDA, Hassan Omar Sarai, kufuatia semi zake zilizoibua utata. Hii ni baada baadhi ya viongozi kutoka eneo la Mlima Kenya kushinikiza Katibu mkuu huyo wa UDA ajiuzulu kutoka wadhifa wake kwa madai ya   semi zake zinachochea ukabila. Wakiongozwa na mwanaharakati wa kisiasa Said Twaha wamesema kuwa kauli za Sarai zilikuwa zinalenga kutetea haki za wakazi wa Pwani waliopokonywa mashamba yao, na wala hazikulenga kuchochea jamii yoyote kama inavyodaiwa na baadhi ya viongozi hao. Twaha amesema wataendelea kusimama kidete na Katibu Mkuu huyo wa UDA kwa kuwa amekuwa nguzo muhimu ya umoja na mshikamano wa amani katika eneo la Pwani. Aidha, amemhakikishia Rais kuwa watafanya kila juhudi kuhakikisha chama cha UDA kinapata asilimia 100 ya kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. “Hassan Sarai ameongea kutetea watu wake WA pwani na hakuchochea ukabila,sisi tumeishi Kwa amani tangu ...

Mwanahamisi Hamadi aadhimisha siku ya usafi wa hedhi na wanafunzi wa kike Likoni.

Image
  Mwanahabari maarufu na mwanzilishi wa Waqf    wa Taji Langu,Mwanahamisi Hamadi, ameungana na wasichana wa shule mbalimbali za Likoni kuadhimisha siku ya Usafi wa Hedhi Duniani. Akizungumza    katika shule ya msingi ya Shikaadabu,Mwanahamisi amesema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuwapatia wasichana wanaosoma elimu kuhusu hedhi na usafi wa hedhi pamoja na jinsi jamii inaweza kushirikiana kupambana na unyanyapaa unaozunguka suala hilo. “Umuhimu wa hafla hii hauko tu katika kuwa mpango wa kiafya, bali pia ni hatua muhimu katika kuendeleza heshima na elimu ya mtoto wa kike. Kwa kuhimiza mazungumzo ya wazi na kutoa taarifa muhimu, tunalenga kuwawezesha wavulana na wasichana kwa maarifa yatakayowasaidia kusimamia afya ya hedhi kwa kujiamini tena bila aibu,” alisema mwanahabari huyo. Mwanahamisi amesema amefurahia kupata nafasi ya kugawa sodo kwa wanafunzi hao ili kuhakikisha kuwa wakati wa hedhi, wasichana wanaweza kushiriki kikamilifu katika masomo yao bila usumbufu...