Posts

Showing posts from September, 2026

Serikali Yaweka Zaidi ya Bilioni 721katika Ujenzi wa Nyumba za Bei Nafuu.

Image
       Serikali imewekeza fedha ya takriban Shilingi bilioni 731.5 katika mikataba ya ujenzi wa zaidi ya nyumba 280,000 zinazoendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali nchini kupitia Mpango wa Nyumba za Bei Nafuu. Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa kongamano la Kila mwaka la chama Cha wasanifu mijengo nchini AAK 2026 iliyofanyika Diani, Kaunti ya Kwale,  Kaimu Katibu wa Nyumba katika Idara ya Serikali ya Nyumba na Maendeleo ya Miji QS Cassius Kusienya, MBS,akiwakilisha na kusoma hotuba ya Katibu Charles Hinga amesema takwimu hizo zimetolewa katika taarifa ya hivi karibuni ya sekta na Principal Secretary Charles M. Hinga. Kwa mujibu wa hotuba hiyo, mpango huo kwa sasa unaendelea katika takriban kaunti 40, huku Serikali ikilenga kuufikisha katika kaunti zote nchini. Serikali pia imesema inalenga kuhakikisha kila eneo bunge kati ya 290 nchini linapata angalau nyumba 220, ikiwa sehemu ya mpango mpana wa kuongeza usambazaji wa nyumba za bei nafuu. Ku...

Wataalamu Wajadili Mustakabali wa Miji Katika Kongamano la chama Cha AAK Kwale.

Image
       Wataalamu na wadau wa sekta ya ujenzi wamekutana Diani, Kaunti ya Kwale, kwa Kongamano la Kila mwaka la chama Cha wasanifu mijengo nchinin (AAK), linalolenga kujadili namna ya kuifanya sekta ya mazingira yaliyojengwa kuwa himilivu dhidi ya changamoto za sasa na zijazo. Kongamano hilo linafanyika Diani kaunti ya Kwale, chini ya kaulimbiu “Shifting the Built Environment from Fragility to Resilience”. Kongamano hilo ni mkutano mkuu wa kila mwaka unaowaleta pamoja wataalamu na wadau kutoka sekta ya mazingira yaliyojengwa kujadili masuala yanayoathiri taaluma, sera pamoja na mustakabali wa miji na jamii. Akizungumza kwa niaba ya Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Idara ya Nyumba na maendeleo ya miji,Kaimu Katibu wa Nyumba katika Idara ya Serikali ya Nyumba na Maendeleo ya Miji QS Cassius Kusienya, MBS, amesema kaulimbiu ya mwaka huu inaakisi hali halisi inayokabili Kenya, huku miji ikikua kwa kasi kuliko mifumo inayohudumia wakazi.     Kw...

ODM Mombasa Yawaonya viongozi wa UDA kukoma Kuwashambulia Viongozi Wao.

Image
      Viongozi wa Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kaunti ya Mombasa wamewataka wenzao wa United Democratic Alliance (UDA) kukoma kuwashambulia  na kuwakosoa viongozi wa ODM, wakisema vyama hivyo ni washirika katika serikali jumuishi na Wala si maadui. Wakizungumza katika kaunti ya Mombasa,wakiongozwa na Mwenyekiti wao katika kaunti hiyo Mohamed Hamid Khamis amesema viongozi na wanachama wa ODM katika kaunti hiyo wamekuwa wakihamasisha wananchi kumuunga mkono Rais William Ruto na kueleza ajenda zake za maendeleo anapolenga kuwania muhula wa pili wa urais.     Khamis amehoji sababu ya baadhi ya viongozi wa UDA kulenga kuwashambulia viongozi wa ODM badala ya kushirikiana katika kuwasilisha ajenda ya serikali jumuishi. “Tunawauliza wenzetu wa UDA, sisi ni maadui wenu ama ni washirika wenu?” Khamis ameuliza. Amesema chama Cha  ODM Mombasa kitaendelea kuwahamasisha wanachama wake kumuunga mkono Rais Ruto, akisisitiza kuwa c...

Sarai Atetea Kauli ya Wafu Kupiga Kura, Awasihi Wakaazi wa Mombasa Kujitokeza Kupiga Kura.

Image
        Katibu Mkuu wa chama Cha United Democratic Alliance (UDA), Hassan Omar Sarai, ametetea kauli yake inayodaiwa kuwa na utata kuhusu wapiga kura waliokufa, akisema ilikuwa ni tamathali iliyolenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika usajili wa wapiga kura. Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Sarai amesema kauli zake zilikuwa na maana ya kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao. Sarai ameshutumu viongozi wa upinzani kwa kupotosha kauli zake na kuzitumia kama propaganda za kisiasa.     Amesema wapinzani wanapotosha kauli zake kwa sababu hawana ajenda ya maendeleo ya kuwaeleza wananchi na wanahofia kushindwa na chama tawala katika uchaguzi ujao. Sarai amesema matumizi ya lugha hiyo yalilenga kuhakikisha kila kura inahesabiwa katika uchaguzi ujao, huku akionyesha imani kuwa Rais William Ruto atashinda na kupata muhula wa pili. Hata hivyo katibu Mkuu huyo wa UDA ame...

Mzozo wa Umiliki wa Ardhi ya Shilingi Bilioni 1.5 Wazuka Samburu kaunti ya Kwale.

Image
         Mgogoro wa umiliki wa shamba lenye ukubwa wa ekari 3,100 na thamani ya Shilingi bilioni 1.5 umezuka eneo la Samburu, Kaunti ya Kwale, huku aliyekuwa mwakilishi wadi Saidi Mung’aro Nzuga na Rev. Fredrick Kanato Ndaikwa wakidai kuwa wao ndio wamiliki halali wa ardhi hiyo. Nzuga amesema yeye pamoja na Kanato walinunua shamba hilo kutoka kwa familia ya Mwachizi mwaka 2018, wakidai kuwa walifuata taratibu zote za kisheria na kufikia makubaliano rasmi na familia hiyo. Amesema wana nyaraka na barua mbalimbali zinazothibitisha kuwa walipata ardhi hiyo kihalali. Aidha, amefichua kuwa hati ya umiliki wa ardhi hiyo ilitolewa mwezi Aprili mwaka huu, baada kuhangaika kwa muda wa miaka Saba.           Hata hivyo, Nzuga anadai kuwa mhandisi Lung’azi Chai, ambaye analenga kuwania ugavana wa Kaunti ya Kwale, amejitokeza na kudai kuwa alinunua shamba hilo mwaka 2024 na kwamba ndiye mmiliki halali. Nzuga anadai kuwa Lung’az...

Familia Moja Samburu Yaililia Serikali Kulipwa Fidia ya Shamba Baada ya Miaka Miwili.

Image
    Familia ya Gari Kambe kutoka eneo la Samburu wadi ya Chengoni kaunti ya Kwale, imeitaka Serikali kuharakisha malipo ya fidia ya shamba lao lenye ukubwa wa ekari 98, ambalo walikubaliana kuliuza kwa Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa EPZ A Samburu. Kwa mujibu wa mwanafamilia, Ndaikwa Jumaa, familia hiyo ilifikia makubaliano na Serikali ya kuuza shamba hilo kwa bei ya shilingi 100,000 kwa kila ekari. Hata hivyo, Ndaikwa amesema licha ya makubaliano hayo, tayari miaka miwili imepita bila familia hiyo kupokea malipo yoyote. Familia hiyo sasa inaitaka Serikali kuingilia kati na kuhakikisha inalipwa fedha zake kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa. Ndaikwa amesema familia imetoa muda wa mwezi mmoja kwa Serikali kushughulikia suala hilo, ikionya kuwa iwapo haitalipwa ndani ya muda huo, italazimika kuchukua hatua zaidi ikiwemo kurejea katika shamba hilo na kuendelea na shughuli zao za ukulima. Familia hiyo ikiwa na Imani Serikali itaingilia kati kwa haraka ...

TotalEnergies Yazindua Kadi Mpya ya Malipo ya Kidijitali Nchini Kenya.

Image
       Wamiliki wa magari na wafanyabiashara nchini Kenya sasa wanaweza kufuatilia na kudhibiti matumizi ya mafuta kwa urahisi zaidi, kufuatia kuzinduliwa kwa mfumo mpya wa malipo wa kidijitali wa TotalEnergies Marketing Kenya. Kampuni hiyo imezindua Kadi Mpya ya TotalEnergies, inayolenga kuboresha usimamizi wa matumizi ya mafuta na kutoa njia salama na rahisi zaidi za kufanya malipo.       Kadi hiyo ni mageuzi ya bidhaa ambayo imekuwa katika soko la Kenya kwa zaidi ya miaka 25, baada ya kuanzishwa kama Bon Voyage Fuel Card, iliyokuwa kadi ya kwanza ya mafuta nchini Kenya na pia ya kwanza kutumia teknolojia ya chip. Kwa sasa, huduma hiyo imepanuliwa kuwa jukwaa kamili la kidijitali la malipo na huduma za usafiri kwa biashara, wasimamizi wa magari pamoja na madereva binafsi. Uzinduzi huo unafanyika wakati ambapo wafanyabiashara nchini wanazidi kutafuta njia bora za kufuatilia na kudhibiti matumizi ya mafuta kutokana na kuongezeka...

Serikali yaharakisha utekelezaji wa mradi wa bilioni 75 WA Dongo Kundu,Yalenga ukamilike 2028.

Image
       Serikali imeongeza kasi ya utekelezaji wa mradi wa Dongo Kundu Special Economic Zone (SEZ),huku wawekezaji 94 wakiwa wamewasilisha maombi ya kuwekeza katika eneo hilo. Katibu katika Wizara ya Uchukuzi, Mohamed Daghar amesema zaidi ya taasisi 10 za serikali zimefanya ukaguzi wa mradi huo wa kimkakati ili kutathmini maendeleo yake na kushughulikia changamoto zinazoweza kuchelewesha utekelezaji wake. Amesema mradi huo wenye thamani ya Shilingi Bilioni 75 unahusisha ujenzi wa gati, barabara, miundombinu ya umeme na maji. Mamlaka ya Bandari Nchini (KPA) inajenga gati la kwanza kati ya saba, lenye urefu wa mita 300, ambalo litawezesha meli kubwa ikiwemo Panamax kutia nanga katika eneo hilo.      Kwa sasa, ujenzi wa gati hilo umefikia asilimia 16, huku KPA ikisema kazi iko mbele ya ratiba kwa takribani asilimia mbili.Mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2028,ila serikali inalenga kuharakisha utekelezaji wake ukamilik...

Ujenzi wa kiwanda Cha gesi Dongo Kundu wafikia asilimia 85.

Image
    Ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuhifadhi gesi ya kupikia kinachojengwa na kampuni ya Taifa Gas kutoka Tanzania katika Eneo Maalum la Kiuchumi la Dongo Kundu umefikia asilimia 85. Mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 15, unajumuisha matangi 12 ya kuhifadhi gesi, ambapo kila tanki lina uwezo wa kuhifadhi tani 2,500,hivyo kutoa uwezo wa jumla wa kuhifadhi tani 30,000. Akizungumza wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo,katibu katika idara ya uchukuzi Mohamed Daghar amesema kampuni ya Taifa Gas ni mwekezaji wa kwanza kuanzisha kituo kikubwa cha aina hiyo katika eneo hilo. Daghar amesema kituo hicho kitakuwa kikubwa zaidi nchini Kenya na katika ukanda wa Afrika, huku kikitarajiwa kuchangia kupunguza bei ya gesi kwa kuwezesha kununuliwa kwa wingi, kuhifadhiwa nchini na kusambazwa katika soko la Kenya pamoja na nchi jirani.              Akiweka wazi kuwa gharama ya nishati nchini imekuwa juu, lakini uwe...

Kaunti ya Mombasa kunufaika na Miradi ya Nyumba za Bei Nafuu ya Bilioni 30.

Image
                           Kaunti ya Mombasa inatarajiwa kunufaika na miradi ya nyumba za bei nafuu yenye thamani ya takriban Shilingi Bilioni 30, hatua inayolenga kubadilisha sura ya jiji hilo la kitalii na kuhakikisha wakazi wanapata makazi ya kisasa na yanayomudu gharama. Akizungumza mjini Mombasa wakati wa zoezi la kupeana ufahamu Kwa jamii kuhusu mradi wa nyumba za bei nafuu Mkurugenzi wa Uratibu wa Kanda ya Pwani, Idara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji John Karanja, amesema serikali inawekeza katika miradi ya nyumba za bei nafuu, masoko na hosteli za wanafunzi ili kukabiliana na uhaba wa makazi jijini Mombasa.                                   Karanja amesema nyumba hizo zitawanufaisha maelfu ya watu wanaofanya kazi Mombasa lakini hulazimika kuutafuta makazi katika Kaunti jirani. Miongoni mwa miradi hiyo ni Mradi wa Nyumba za Bei ...

WAKAAZI WA MVITA WAHIMIZWA KUJISAJILI NA KUNUNUA NYUMBA ZA BEI NAFUU.

Image
                                    Mbunge wa Mvita, Mohamed Sudi Machele, amewataka wakazi wa eneo hilo kuchangamkia mpango wa serikali wa nyumba za bei nafuu kupitia mradi wa Boma yangu, akisema takriban nyumba 1,800 zinatarajiwa kujengwa katika eneo hilo. Machele amesema ameandaa zoezi maalum la kuwaelimisha wakazi kuhusu namna ya kutuma maombi na kunufaika na nyumba hizo, akisema wengi bado hawajafahamu mchakato huo. Amesema mradi wa Makupa Market utakuwa na soko pamoja na nyumba za makazi.                               Amesema mipango mingine inalenga Old Town, ambako kutajengwa soko la samaki la ghorofa tatu pamoja na nyumba za makazi. Ameongeza kuwa miradi hiyo itatekelezwa kwa awamu, huku kila mradi ukiwa na mkataba na muda wake wa kukamilika. Machele amesema wanufaika hawatalazimika kulipa gharama yote ya nyum...

KTDA Yasafirisha Tani 99,000 za Mbolea kupitia SGR Kuwafikia Wakulima wa majani Chai.

Image
              Shirika la KTDA limeanza kusafirisha tani 99,000 za mbolea kutoka Bandari ya Mombasa hadi Nairobi kupitia reli ya kisasa (SGR), kwa ajili ya usambazaji kwa wakulima wa majani chai nchini. Mwenyekiti wa Kitaifa wa KTDA, Enos Njeru EGH, amesema shehena hiyo imeagizwa kupitia zabuni ya kimataifa kwa niaba ya zaidi ya wakulima 650,000. Meli ya kwanza kati ya tatu imewasili Mombasa Septemba 3, huku mbili zikitarajiwa kufika ndani ya mwezi huu. Baada ya kufungashwa, shehena hiyo itazalisha takribani mifuko milioni 1.9 ya mbolea aina ya NPK 26:5:5, kila mmoja ukiwa na uzito wa kilo 50. Kiasi hicho kimeongezeka kutoka tani 93,000 mwaka 2023.         Njeru amesema matumizi ya SGR yatawezesha mbolea kusafirishwa kwa haraka na kwa ufanisi kutoka Mombasa hadi Nairobi, kabla ya kusafirishwa kwa barabara hadi viwandani ambako itagawiwa kwa wakulima walioagiza. Amesema shirika la KTDA linalenga kuhakikisha wak...

Mombasa Yaongeza Maandalizi Kukabiliana na Mvua za Elnino Zilizotabiriwa.

Image
            Kaunti ya Mombasa imeimarisha maandalizi ya kukabiliana na mvua kubwa zinazotarajiwa katika miezi ijayo, huku Gavana Abdullswamad Sheriff Nassir akiweka wazi kuwa kaunti hiyo lazima ichukue hatua mapema ili kupunguza hatari ya mafuriko na vifo. Akizungumza baada ya kikao cha Kamati ya Pamoja ya Maandalizi ya Maafa, Nassir amesema utabiri wa hali ya hewa unaonyesha uwezekano mkubwa wa kutokea kwa mvua ya El Niño, huku mvua zikitarajiwa kuwa kubwa zaidi na kudumu kwa muda mrefu ikilinganishwa na matukio ya awali. Amesema mvua hizo zinatarajiwa kuanza kuelekea mwishoni mwa Septemba na kuendelea kwa miezi kadhaa, huku hali ya kuwepo na mvua ikitarajiwa kuendelea hadi Januari na Februari.               Kwa mujibu wa Gavana huyo, kiwango cha mvua kinaweza kufikia hadi milimita 680, kiwango ambacho ni kikubwa zaidi ikilinganishwa na mvua zilizoshuhudiwa wakati wa matukio ya El Niño ya mwaka 202...

Mbunge Feisal Bader Atuhumiwa Kuzuia Msambweni Talent Show Kufanyika Mvindeni Youth Centre.

Image
    Waandalizi wa Msambweni Talent Show wamemtuhumu Mbunge wa Msambweni, Faisal Badar, kwa kuzuia matumizi ya Mvindeni Youth Opportunity Center, ambako hafla hiyo ilikuwa imeratibiwa kufanyika. Mmoja wa waandalizi wa shughuli hiyo, Hassan Madzaya, amesema walifika mapema na walikuwa wamelipia ukumbi huo, lakini walizuiwa kuingia kwa madai kuwa mbunge huyo aliwaelekeza wasimamizi kuwazuia na kutoruhusu shughuli hiyo kufanyika hapo. Iliwalazimu waandalizi kuweka mahema na viti nje ya kituo hicho, na hafla ikaendelea kama ilivyoratibiwa.         Hassan amesema mpango huo unalenga kukuza vipaji vya vijana katika soka, muziki, ushairi, uandishi wa habari na utengenezaji wa maudhui ya kidijitali, pamoja na kuwasaidia vijana kupata kipato kupitia uchumi wa kidijitali. Akisema kitendo Cha kuwazuia kuingia katika kituo hicho si Cha kiungwana na kinaregesha nyuma juhudi za vijana kutizima ndoto zao kupitia vipaji. Mwaniaji wa kiti Cha ubu...