Serikali Yaweka Zaidi ya Bilioni 721katika Ujenzi wa Nyumba za Bei Nafuu.

      

Serikali imewekeza fedha ya takriban Shilingi bilioni 731.5 katika mikataba ya ujenzi wa zaidi ya nyumba 280,000 zinazoendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali nchini kupitia Mpango wa Nyumba za Bei Nafuu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa kongamano la Kila mwaka la chama Cha wasanifu mijengo nchini AAK 2026 iliyofanyika Diani, Kaunti ya Kwale,  Kaimu Katibu wa Nyumba katika Idara ya Serikali ya Nyumba na Maendeleo ya Miji QS Cassius Kusienya, MBS,akiwakilisha na kusoma hotuba ya Katibu Charles Hinga amesema takwimu hizo zimetolewa katika taarifa ya hivi karibuni ya sekta na Principal Secretary Charles M. Hinga.

Kwa mujibu wa hotuba hiyo, mpango huo kwa sasa unaendelea katika takriban kaunti 40, huku Serikali ikilenga kuufikisha katika kaunti zote nchini.

Serikali pia imesema inalenga kuhakikisha kila eneo bunge kati ya 290 nchini linapata angalau nyumba 220, ikiwa sehemu ya mpango mpana wa kuongeza usambazaji wa nyumba za bei nafuu.

Kusienya amesema zaidi ya Wakenya milioni moja wamejisajili kwenye mfumo wa Boma Yangu, huku takriban maombi 545,000 ya ugawaji wa nyumba yakiwa tayari kwenye mfumo.

Hata hivyo, alisema usajili pekee haupaswi kuchukuliwa kuwa umiliki wa nyumba, akisisitiza umuhimu wa kuunganisha mchakato wa usajili na ugawaji, ufadhili, makazi na hatimaye hati miliki.

Hotuba hiyo ilieleza kuwa nyumba za kijamii zimekuwa zikitolewa kwa bei ya Shilingi 640,000 kwa chumba kimoja, 960,000 kwa vyumba viwili na milioni 1.28 kwa vyumba vitatu.

    

Kwa upande wa nyumba za bei nafuu, nyumba aina ya studio imeorodheshwa kwa bei y Shilingi milioni 1 huku nyumba ya vyumba viwili ikiwa Shilingi milioni 2.

Idara ya Serikali ya Nyumba na Maendeleo ya Miji imewajulisha wanaotuma maombi  kuwa bei hizo zitapitiwa upya kuanzia Oktoba 1, 2026, huku waombaji watakaokamilisha mgao chini ya bei za sasa wakihifadhiwa bei hiyo.

Kusienya amesema mpango huo pia unalenga kuchochea ajira na uzalishaji wa ndani, huku zaidi ya ajira 640,000 zikitajwa kuwa zimehusishwa na mnyororo wa thamani wa sekta ya nyumba.

Serikali ikitaka nyumba zijengwe kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi

Akizungumza kuhusu kauli mbiu ya mkutano huo “Shifting the Built Environment from Fragility to Resilience,” Kusienya amesema ujenzi wa nyumba haupaswi kuangaliwa kwa idadi pekee, bali pia ubora, eneo, huduma, uwezo wa kumudu gharama na uimara wake.

Akisema nyumba zinapaswa kujengwa katika maeneo yenye maji, usafi, mifereji ya maji, nishati, barabara na huduma nyingine muhimu.

Kwa mujibu wa hotuba hiyo, mabadiliko ya tabianchi tayari yanaonekana kupitia mafuriko, joto katika majengo, barabara kuharibika na changamoto nyingine za mijini.

Akisisitiza umuhimu wa kutumia mbinu za ujenzi zinazozingatia mazingira, ikiwemo paa zinazopunguza joto, uingizaji hewa wa asili, matumizi ya vifaa vinavyoweza kurejelewa na mipango ya maeneo inayozingatia maji.

Amesema uzoefu wa maeneo ya Pwani, ikiwemo Kwale, unaweza kusaidia katika kubuni nyumba zinazolingana na hali ya hewa, upepo na mazingira ya ukanda wa pwani.

Serikali imewataka wataalamu katika sekta ya ujenzi, wakiwemo wasanifu majengo, wapima ardhi, wahandisi na wasimamizi wa miradi, kushirikiana katika kuhakikisha nyumba zinazojengwa zinakuwa salama, nafuu na endelevu.

Kusienya amesema wataalamu hao wana jukumu la kusaidia kupunguza gharama za ujenzi bila kuathiri ubora, pamoja na kuongeza matumizi ya vifaa vya ndani na kushirikisha makandarasi wadogo na sekta ya Jua Kali.

Akiweka wazi kuwa kuna haja ya kuharakisha mchakato wa kuwabadilisha waliosajiliwa kwenye Boma Yangu kuwa wamiliki wa nyumba kupitia ufadhili, makazi na hati miliki.

Akisisitiza mafanikio ya mpango wa nyumba hayapaswi kupimwa kwa idadi ya majengo pekee, bali kwa uwezo wa nyumba hizo kuwa makazi yanayoweza kumudu gharama, yenye huduma, yanayostahimili mabadiliko ya tabianchi na hatimaye kuwa mali ya wakaazi.

Comments

Popular posts from this blog

Viongozi wa Kidini PPRL Waunga Mkono Agizo la wizara ya elimu la Ratiba ya Masomo Shuleni

Mbunge Feisal Bader Atuhumiwa Kuzuia Msambweni Talent Show Kufanyika Mvindeni Youth Centre.

Kaunti ya Wajir yaandaa Sherehe za Madaraka Day kwa mara ya kwanza tangu Kenya ipate Uhuru.