Mbunge Feisal Bader Atuhumiwa Kuzuia Msambweni Talent Show Kufanyika Mvindeni Youth Centre.

   
Waandalizi wa Msambweni Talent Show wamemtuhumu Mbunge wa Msambweni, Faisal Badar, kwa kuzuia matumizi ya Mvindeni Youth Opportunity Center, ambako hafla hiyo ilikuwa imeratibiwa kufanyika.

Mmoja wa waandalizi wa shughuli hiyo, Hassan Madzaya, amesema walifika mapema na walikuwa wamelipia ukumbi huo, lakini walizuiwa kuingia kwa madai kuwa mbunge huyo aliwaelekeza wasimamizi kuwazuia na kutoruhusu shughuli hiyo kufanyika hapo.

Iliwalazimu waandalizi kuweka mahema na viti nje ya kituo hicho, na hafla ikaendelea kama ilivyoratibiwa.
  
    
Hassan amesema mpango huo unalenga kukuza vipaji vya vijana katika soka, muziki, ushairi, uandishi wa habari na utengenezaji wa maudhui ya kidijitali, pamoja na kuwasaidia vijana kupata kipato kupitia uchumi wa kidijitali.

Akisema kitendo Cha kuwazuia kuingia katika kituo hicho si Cha kiungwana na kinaregesha nyuma juhudi za vijana kutizima ndoto zao kupitia vipaji.

Mwaniaji wa kiti Cha ubunge wa Msambweni wakili Salim Ali Mwadumbo, ametetea uamuzi wa waandalizi kuendelea na hafla hiyo nje baada ya kudaiwa kuzuiwa kutumia ukumbi waliokuwa wameweka licha ya kuilipia.

Mwadumbo amesema ukumbi huo ulilipiwa Agosti 31, 2026, na waandalizi wakapewa risiti ya kuthibitisha malipo ya ukodishaji.
           

Akisema vituo vya umma vinapaswa kuwa wazi kwa wanajamii wote bila kujali misimamo ya kisiasa, akiwataka viongozi kuunga mkono mipango inayolenga kukuza vipaji vya vijana.

Amesema takribani vijana 80 wamejisajili kushiriki mashindano hayo, yenye Nyanja mbalimbali ya vipaji.

Kiongozi huyo pia amesisitiza kuwa mpango huo unalenga vijana na vipaji vyao, wala si siasa, akisema lengo ni kuwapa vijana fursa za kukuza vipaji na kujikwamua kiuchumi.

         

Mwadumbo pia ameweka wazi azma yake ya kuwania kiti cha ubunge wa Msambweni katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, akiahidi kuboresha maisha ya wananchi na kukuza vipaji vya vijana.
Akiwataka vijana kutokata tamaa na kushirikiana katika kuleta mabadiliko ya uongozi.

Kwa upande wao, vijana wakiongozwa na msanii Halima Kingi walilalamikia kufungwa kwa ukumbi huo, wakisema hatua hiyo inakatisha tamaa vijana wanaotegemea sanaa kujiendeleza.
         

Nae Said Boi msanii kutoka Diani amesema viongozi wanapaswa kuwawezesha vijana badala ya kuwawekea vikwazo, huku Sawa Salim, anayelenga kuwania useneta wa Kwale, akiahidi kuanzisha vituo vya vijana kupitia ushirikiano na wawekezaji iwapo atachaguliwa.

Mtengeneza maudhui Bujra Mohamed aliwataka vijana kuendelea kujikita katika Sanaa kwani inalipa vizuri iwapo utatumia fursa zako vyema.

        

Bujra pia amedai ukumbi huo ni wa umma na vijana wanapaswa kupewa fursa ya kuutumia bila vikwazo vya kisiasa.

Msambweni Talent Show itaendelea kwa awamu hadi Desemba 2026, ambapo fainali inatarajiwa kufanyika.

Mshindi wa kwanza ataondoka na shilingi laki tano huku wa pili akiondoka na laki tatu na mshindi wa tatu akitia kibindoni pesa taslim shilingi laki mbili na zawadi zengine kemkem.

Comments

Popular posts from this blog

Viongozi wa Kidini PPRL Waunga Mkono Agizo la wizara ya elimu la Ratiba ya Masomo Shuleni

Kaunti ya Wajir yaandaa Sherehe za Madaraka Day kwa mara ya kwanza tangu Kenya ipate Uhuru.