Sportpesa National 7s Circuit:KCB yatinga robo Fainali Kwa kishindo.
KCB ilianza kampeni kwa ushindi wa alama 22-5 dhidi ya Kisumu RFC, kabla ya kuishinda Uganda Emerging 7s kwa alama 12-7 katika mchezo wa pili. Katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi, KCB iliibuka na ushindi wa alama 29-10 dhidi ya KU Black Blad, na hivyo kufuzu kwa robo fainali itakayochezwa Jumapili.
Kabras Sugar walimaliza katika nafasi ya pili baada ya pia kutokupoteza mchezo. Waliifunga wenyeji Mombasa Sports Club Rugby kwa 43-0, kisha wakashinda Nondescripts RFC kwa 12-0. Hata hivyo, walilazimishwa sare ya 17-17 na Kenya Harlequins katika mchezo wao wa mwisho.
NYS Spades nao wameweka historia kwa kufuzu kwa mara ya kwanza katika robo fainali SPORTPESA National 7s Circuit. Spades walianza kwa sare alama 5-5 dhidi ya Mwamba RFC, kisha wakapata ushindi muhimu wa alama 15-12 dhidi ya Strathmore Leos, kabla ya kuifunga MMUST Rugby kwa alama 7-5 na kufuzu hatua ya robo fainali.
Katika Pool A, Kabras RFC waliendelea na kiwango chao kizuri kwa kumaliza bila kupoteza mchezo na kuongoza kundi, huku Nondescripts wakimaliza nafasi ya pili.
Menengai Oilers walitawala Pool C baada ya kushinda michezo yote mitatu. Walianza kwa kuifunga Nakuru RFC alama 14-7, wakawachapa wenyeji Kilifi RFC alama 34-5 na kumalizia kwa ushindi wa alama 31-5 dhidi ya Daystar Falcons.
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa wa Mahusiano ya Umma , Mauzo na Matangazo katika Katika Kampuni ya SportPesa Mercy Kabui amesema mwaka huu mgao wa zawadi umeongezwa maradufu, huku washindi katika vitengo mbalimbali wakipangiwa donge nono.
Amesema hatua hiyo itasaidia kutoa hamasa kwa timu zinazoshiriki, pamoja na kuwasaidia wachezaji kujikimu kimaisha.
Aidha, Mercy amefichua kuwa kuna wataalamu maalum wanaofuatilia vipaji vinavyochipuka, kwa lengo la kubaini wachezaji wenye uwezo na kuwapa fursa ya kujiunga na timu ya taifa ya raga nchini Shujaa.
Akiwataka washiriki kujituma kikamilifu ili kuonyesha uwezo wao, kujitangaza na kutambuliwa na wale wanaofuatilia vipaji.
Mercy pia amesema mwitikio wa mashindano hayo umekuwa mkubwa, huku akiwahimiza mashabiki kujitokeza kwa wingi zaidi.
Michezo ya robo fainali pamoja na mechi nyingine za mtoano itachezwa Jumapili
Comments
Post a Comment