MOMBASA MEGA MARATHON YAZINDULIWA, ZAIDI YA WASHIRIKI 1,000 WATHIBITISHA USHIRIKI WAO.
Makamu wa Kwanza
wa Rais wa shirikisho hilo, Paul Mutwii, amezindua mashindano hayo jijini
Mombasa Jumatatu, akimwakilisha Rais wa shirikisho hilo Jenerali Mstaafu
Jackson Tuwei.
Mutwii
amesema wamefurahishwa na kurejea kwa mashindano makubwa ya Marathon Mombasa,
baada ya kutokuwepo kwa miaka kadhaa.
Amesema Rais
wa huyo amesaini kibali cha mashindano hayo, huku waandaaji wakitarajiwa
kukabidhiwa kibali hicho wakati wa uzinduzi.
Mashindano
hayo yatakuwa na mbio za kilomita 42, kilomita 21, kilomita 10 na kilomita 5.
Balozi wa
Mombasa Mega Marathon, Omar Said, amesema zaidi ya washiriki 1,000 tayari
wamejisajili kwa mashindano hayo ya kwanza.
Mbio za burudani
za kilomita 5 zinatarajiwa kuanza kati ya saa mbili na nusu na saa tatu
asubuhi.
Said amesema
mbio hizo za burudani zinalenga watoto, wazee, familia na washiriki wengine
ambao hawawezi kukimbia umbali mrefu.
Kwa mujibu
wa Shirikisho la Riadha Nchini, jumla ya shilingi milioni 5.084 zimetengwa kama
zawadi kwa washindi.
Wanariadha
watakaoshinda zawadi watafanyiwa vipimo vya matumizi ya dawa zilizopigwa
marufuku kabla ya fedha zao kutolewa.
Vipimo hivyo
vitaendeshwa na Wakala wa Kitaifa wa Kupambana na Matumizi ya Dawa za Kulevya,
ADAK.
Said amesema
mbio hizo inalenga pia kuhamasisha jamii
ya Mombasa kupinga matumizi ya dawa za kulevya.
Akiongeza
kuwa waandaaji wanatarajia kusaidia
makundi yanayofanya kazi na watu walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya,
kwa kushirikiana na mashirika kama Reachout na Mewa Rehabs.
Naibu Gavana
wa kaunti ya Mombasa, Francis Thoya, amesema michezo inatoa fursa ya
kukabiliana na tatizo la matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana.
Thoya akisema
Mombasa inakabiliwa na changamoto kubwa ya matumizi ya dawa za kulevya,
akieleza kuwa vijana wasio na shughuli za kufanya huwa katika hatari kubwa ya
kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya na matatizo mengine ya kijamii.
Akisema kuna
haja ya kuinua hadhi ya riadha Mombasa na kurejesha enzi ambazo jiji hilo
lilikuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya riadha.
Kaunti ya
Mombasa itasaidia mashindano hayo kwa kutoa usalama na huduma nyingine muhimu.
Afisa wa
kiufundi wa Shirikisho la Riadha Nchini, James Mwaringa, amesema Bustani ya Mama
Ngina Waterfront itakuwa eneo la kuanzia na kumalizia mashindano hayo.
Eneo hilo
pia litatumika kama Race Village, ambapo shughuli mbalimbali za mashindano
zitafanyika.





Comments
Post a Comment