Mpango wa Marupurupu kwa Wazee wa Vijiji Kuimarisha Utawala wa Mashinani.



Serikali ya Kitaifa imepongezwa kwa uamuzi wa kuanza kuwalipa wazee wa vijiji marupurupu ya kila mwezi, hatua inayolenga kuimarisha ushirikiano wao na machifu pamoja na vyombo vya usalama katika kutekeleza majukumu ya kiutawala na kudumisha usalama mashinani.

Akizungumza Mombasa, Kamishina wa Kaunti hiyo, Mohamed Noor Hassan, amesema marupurupu hayo yatawasaidia wazee wa vijiji kukidhi mahitaji yao ya kimsingi huku yakitambua mchango wao mkubwa katika kuhudumia jamii.

Amesema wazee wa vijiji ni kiungo muhimu kati ya wananchi na serikali, wakichangia kwa kiasi kikubwa katika ukusanyaji wa taarifa za kiusalama, utatuzi wa migogoro na kuimarisha utawala bora katika ngazi ya jamii.
            

Wakati huo huo, Kamishina Noor amewataka wazazi kuwa waangalifu na kuwafuatilia watoto wao wakati wa likizo ya shule ili kuwakinga dhidi ya ushawishi wa makundi ya uhalifu na vitendo vingine vinavyoweza kuhatarisha usalama wao.
 
Amesisitiza kuwa vyombo vya usalama vimeimarisha doria na viko tayari kukabiliana kikamilifu na wahalifu watakaojaribu kuvuruga amani.


Mapema wiki hii, Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama wa Ndani, Raymond Omollo, aliongoza kikao cha wadau wa sekta ya usalama katika Kaunti ya Mombasa kuzindua utekelezaji wa mpango huo.

Kikao hicho kilijadili hali ya usalama katika ukanda wa Pwani na kusisitiza umuhimu wa kushirikiana kukabiliana na magenge ya uhalifu, biashara ya dawa za kulevya pamoja na usambazaji wa taarifa za upotoshaji zinazoweza kuhatarisha usalama wa taifa.
        

Comments

Popular posts from this blog

Viongozi wa Kidini PPRL Waunga Mkono Agizo la wizara ya elimu la Ratiba ya Masomo Shuleni

Mbunge Feisal Bader Atuhumiwa Kuzuia Msambweni Talent Show Kufanyika Mvindeni Youth Centre.

Kaunti ya Wajir yaandaa Sherehe za Madaraka Day kwa mara ya kwanza tangu Kenya ipate Uhuru.