SISI NI DOLA CUP: Ushindani Mkali Kutarajiwa Hatua ya 16 Bora.

        

Timu ya Mombasa Sports Club imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Wonderers katika mchezo wa Sisi Ni Dola Super Cup uliochezwa katika Uwanja wa Mombasa Sports Club.

Sudi Morris alifungua ukurasa wa mabao dakika ya kwanza, kabla ya Alex Chamwoma kuongeza la pili dakika ya 30. Wonderers walipata bao la kufutia machozi dakika ya 88 kupitia Nassoro Hassan kwa mkwaju wa penalti.

      

Katika mchezo mwingine, Kombani Youth iliifunga Mtwapa All Stars 2-1. Mtwapa walitangulia kupitia Ali Msomali dakika ya pili, kabla ya bao la kujifunga la Alfani Idi dakika ya 13 kusawazisha. Mwinyi Malandi aliifungia Kombani Youth bao la ushindi dakika ya 59.

Nahodha wa Mombasa Sports Club, Madigi, amesema anatarajia ushindani mkubwa katika hatua ya 16 bora, akisema timu zimeonyesha viwango vya juu na anaamini kikosi chake kitafanya vizuri.

         

Kwa upande wake, kocha wa Kombani Youth, Juma Zani, amesema licha ya ratiba kuwa ngumu, wataendelea kujiandaa vyema kukabiliana na wapinzani wao, akisisitiza kuwa timu yake ina uwezo na uzoefu wa kushindana.

Miongoni mwa timu zilizofuzu hatua ya 16 bora ni Green Eagles, Nabada FC, Kombani Youth na Mombasa Sports Club.

Fayaz na Mtwapa All Stars bado zinasubiri kujua hatma yao, huku Magongo na Wonderers FC zikiwa tayari zimeaga mashindano.

Comments

Popular posts from this blog

Viongozi wa Kidini PPRL Waunga Mkono Agizo la wizara ya elimu la Ratiba ya Masomo Shuleni

Mbunge Feisal Bader Atuhumiwa Kuzuia Msambweni Talent Show Kufanyika Mvindeni Youth Centre.

Kaunti ya Wajir yaandaa Sherehe za Madaraka Day kwa mara ya kwanza tangu Kenya ipate Uhuru.