Mwaguya Aongoza Katika Kura ya Maoni ya Useneta kaunti ya Mombasa.
Mgombea wa kiti cha Useneta wa Mombasa, Hamisi Mwaguya, ameibuka kinara katika kura ya maoni iliyofanywa na Swiss Polls, akiongoza kwa asilimia 27.2 ya uungwaji mkono, sawa na kura 1,435.
Mwaguya amemshinda kwa tofauti ya asilimia 2.7 mpinzani wake wa karibu, Seneta wa Mombasa Mohamed Faki, aliyepata asilimia 24.5, sawa na kura 1,294.
Uongozi wa Mwaguya katika kura hiyo ya maoni unampa mwanzo mzuri katika mbio za Useneta wa Mombasa, huku akionekana kupata msukumo wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Pia inamuweka katika nafasi ya kuimarisha zaidi uungwaji mkono wake huku kampeni zikitarajiwa kushika kasi.
Mgeni Mboto Hassan ameshika nafasi ya tatu kwa asilimia 10.3, akifuatwa na Bernard William kwa asilimia 9.9 na Victor Abayo kwa asilimia 9.5.
Utafiti huo ulihusisha sampuli ya watu 5,284, una kiwango cha makosa cha pamoja au pungufu asilimia tatu na kiwango cha kuaminika cha asilimia 95.
.
Comments
Post a Comment