MWANI WAGEUKA FURSA YA BIASHARA NA SULUHISHO KWA KILIMO UKANDA WA PWANI

                    


Haarakati zimeanzishwa kuhamasisha matumizi ya kichocheo cha ukuaji wa mimea [Biostimulants]  vinavyotokana na mwani miongoni mwa wakulima katika maeneo ya Pwani ya Kenya.

Mpango huo unaolenga kushirikisha wakulima katika majaribio ya bidhaa hizo pia unakusudia kuwasaidia wanawake wanaokusanya mwani kupata soko la bidhaa zao, huku wakulima wakinufaika na teknolojia inayoweza kuongeza uzalishaji wa mazao na kuyafanya kustahimili changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Thierry Bodson, mshirika wa kiufundi kutoka CASCADIA kwa ushirikiano na shirika la Plan International katika mpango huo, amesema kichocheo cha ukuwaji wa mimea vinaweza kuwa suluhisho la changamoto zinazowakabili wakulima, hususan wakati wa ukame, kupungua kwa rutuba ya udongo na magonjwa ya mimea pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.

Bodson amesema kichocheo cha ukuaji wa mimea zimetumika na wakulima kwa vizazi kadhaa, huku tafiti za hivi karibuni zikionyesha kuwa zinaweza kuwa na manufaa mbalimbali katika uzalishaji wa mazao.

“Biostimulants husaidia mimea kustahimili ukame, kunyonya na kutumia mbolea kwa ufanisi zaidi, na pia husaidia katika ukuaji wa mizizi ya mimea,” amesema Bodson.

Akiweka wazi kuwa Lengo ni kuwawezesha wakulima kufuatilia maendeleo ya mazao na kulinganisha matokeo kabla ya kuamua iwapo bidhaa hizo zinafaa kwa mazingira yao.

Mpango huo pia unalenga kuimarisha fursa za kiuchumi kwa wanawake wanaohusika na ukusanyaji wa mwani katika maeneo ya Pwani.

Akisema badala ya mwani kuuzwa kama malighafi pekee, kuna uwezekano wa kuongezwa thamani kwa kuubadilisha kuwa kichocheo cha ukuaji wa mimea,hivyo kutengeneza soko jipya kwa vyama vya wanawake vinavyokusanya mwani.

Kampuni ya kutengeneza kichocheo cha ukuaji wa mimea imesema bidhaa hiyo husaidia mimea kutumia virutubisho na maji kwa ufanisi zaidi, huku ikisaidia kukabiliana na changamoto za kimazingira kama ukame na chumvi kwenye udongo.

Muhdhar Mohamed, mwalimu na mjasiriamali wa kampuni ya Morganic , amesema kichocheo cha ukuaji wa mimea  husaidia kuimarisha ukuaji wa mizizi na kuongeza uwezo wa mimea kunyonya virutubisho baada ya kuwekwa mbolea.

Amesema kampuni yake ina uwezo wa kuzalisha hadi lita 10,000 kwa mwezi, ingawa kwa sasa uzalishaji ni mdogo kutokana na mahitaji ya soko. Hata hivyo, amesema uhitaji wa kichocheo cha ukuaji wa mimea umeongezeka kwa karibu asilimia 200 tangu mwaka jana.

Akiipongeza Serikali kwa kuimarisha udhibiti wa pembejeo bandia kupitia Organic Farm Inputs and Fertilizer Manufacturers Association of Kenya (OFIMAK).

                               

Amesema kampuni hiyo imefanya majaribio ya kichocheo cha ukuaji wa mimea [biostimulants] katika mazao mbalimbali yakiwemo mahindi, muhogo, nyanya na mboga, huku akiamini teknolojia hiyo inaweza kuongeza uzalishaji wa chakula, hasa maeneo ya Pwani.

Mwangangi kutoka shirika la Plan International amesema biostimulants husaidia kuimarisha mizizi ya mimea na kuongeza uwezo wake wa kutumia virutubisho na maji kwa ufanisi, hasa katika maeneo yenye mvua chache na udongo usio na rutuba.

Akisema mpango huo pia unalenga kuunganisha rasilimali za bahari, hususan mwani, na kilimo kwa kutengeneza bidhaa zenye thamani zaidi, hatua inayoweza kuwafungulia wanawake wanaokusanya mwani fursa za soko na kuwawezesha wakulima kupata suluhisho la ndani dhidi ya changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Fatuma Masudi, mkulima wa mwani kutoka Shimoni, amesema alianza kilimo hicho mwaka 2019 bila kufahamu faida zake, lakini kwa sasa kimekuwa chanzo muhimu cha kipato na kimemwezesha kujenga na kujikimu kimaisha.

Amesema mwani una matumizi mbalimbali, ikiwemo katika bidhaa za afya na kilimo, huku akieleza kuwa watu wengi wameanza kujiunga na kilimo hicho kutokana na faida zake za kiuchumi.

Hata hivyo, amesema changamoto kubwa ni baadhi ya wanunuzi wa awali kuondoka, hali inayowaathiri wakulima.

Fatuma ameiomba Serikali kutafuta masoko ya uhakika na kuwaunganisha wakulima na wanunuzi ili waweze kuuza mwani kwa bei nzuri.


Comments

Popular posts from this blog

Viongozi wa Kidini PPRL Waunga Mkono Agizo la wizara ya elimu la Ratiba ya Masomo Shuleni

Mbunge Feisal Bader Atuhumiwa Kuzuia Msambweni Talent Show Kufanyika Mvindeni Youth Centre.

Kaunti ya Wajir yaandaa Sherehe za Madaraka Day kwa mara ya kwanza tangu Kenya ipate Uhuru.