SISI NI DOLA CUP Makala ya pili yang'oa nanga,Milioni 1 kushindaniwa.

                                                    

Michuano ya Sisi ni Dola Cup makala ya pili kuanza rasmi siku ya Jumamosi katika uwanja wa Mombasa Sports Club, huku mshindi wa kwanza akiondoka na kitita cha Shilingi milioni moja taslimu.

Mashindano hayo yamejumuisha timu 24 zilizofuzu kutoka kwa zaidi ya timu 200 zilizowasilisha maombi ya kushiriki kutoka kaunti tano za Pwani ambazo ni Mombasa, Kwale, Kilifi, Lamu na Tana River.

                                       

Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa Masuala ya Michezo katika Kampuni ya Dola, Hassan Ibrahim, amesema lengo la Sisi ni Dola Cup ni kuwapa vijana fursa ya kuonyesha vipaji vyao na kujitangaza ili wapate nafasi ya kusajiliwa na timu za Ligi Kuu na za kimataifa.

                                       

Amewahimiza washiriki kutumia mashindano hayo ipasavyo kwa kujituma na kuonyesha nidhamu ili kufungua milango ya mafanikio katika soka.

Aidha, Hassan Ibrahim amewataka washiriki kudumisha amani, mshikamano na nidhamu ya hali ya juu, akisema ndiyo msingi wa maendeleo ya mchezo wa soka. 

Akiongeza kuwa lengo lao si tu kuwazawadia washindi, bali pia kuwasaidia wachezaji kupata ufadhili na fursa za kucheza katika viwango vya juu, ikiwemo kimataifa.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Wizara ya Michezo katika Kaunti ya Mombasa, Goshi Juma Ali, ameipongeza Kampuni ya Dola kwa juhudi zake za kutambua na kukuza vipaji vya vijana kupitia mashindano hayo.

                                                

Goshi pia ametoa wito kwa wadau kuendelea kudhamini timu na vipaji vya vijana, akisema hatua hiyo itawasaidia kutimiza ndoto zao na kuwakinga dhidi ya matumizi ya mihadarati pamoja na kujiingiza katika magenge ya uhalifu.

Comments

Popular posts from this blog

Viongozi wa Kidini PPRL Waunga Mkono Agizo la wizara ya elimu la Ratiba ya Masomo Shuleni

Mbunge Feisal Bader Atuhumiwa Kuzuia Msambweni Talent Show Kufanyika Mvindeni Youth Centre.

Kaunti ya Wajir yaandaa Sherehe za Madaraka Day kwa mara ya kwanza tangu Kenya ipate Uhuru.