Raia wa kigeni Washtakiwa kwa Kudaiwa Kusababisha Moto uloharibu mali ya Thamani ya Shilingi Milioni 667.
Mtu mmoja mwenye uraia wa Kenya na Italia anayejulikana kwa jina la Franco Esposito maarufu kama kama Kososo wa Baya na mwenzake Elly Esposito, wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Malindi wakikabiliwa na shtaka la kutochukua tahadhari na kusababisha madhara, kinyume na Kifungu cha 243(d) cha Kanuni ya Adhabu.
Kulingana na hati ya mashtaka iliyowasilishwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) Malindi, washtakiwa hao wanadaiwa kuwa mnamo tarehe 25 Mei 2026 katika eneo la Siro Land, Kaunti Ndogo ya Malindi, Kaunti ya Kilifi, walianzisha moto katika sehemu ya wazi bila kuchukua tahadhari zinazohitajika na wakashindwa kuudhibiti.
![]() |
| Franco Esposito na Elly Esposito wakiwa kizimbani |
Upande wa mashataka unadai kuwa moto huo ulisababisha uharibifu mkubwa wa Duma Villa, mali inayomilikiwa na Nagia Dahmani, yenye thamani inayokadiriwa kuwa Zaidi ya Shilingi milioni 667.
Washtakiwa hao walikamatwa tarehe 6 Julai 2026 na kufikishwa mahakamani, ambapo waliamriwa kuzuiliwa rumande. Kesi hiyo imesajiliwa chini ya Police Case No. 313/2026 na OB No. 11/27/05/2026.
Mlalamishi Nagia Dahmani ambaye pia ni mmiliki wa Duma Villa ni miongoni mwa mashahidi wanaotarajiwa kutoa ushahidi katika kesi hiyo, wengine wakiwa ni pamoja na Samuel Katana, Anderson Mwen, Agnes Mashaka Kaingu, Kingi Karisa, na maafisa kadhaa wa polisi kutoka Malindi.
Tayari uchunguzi uliofanywa na polisi wa Malindi umekamilika, na faili la kesi liko mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
Kesi hiyo inaangazia uzito wa athari zinazoweza kusababishwa na uzembe unaohusisha moto, hasa kwa mali za thamani kubwa katika maeneo ya pwani.




Comments
Post a Comment