Mpango wa PropelA Waanza Mombasa Kuwawezesha Vijana Kupata Ujuzi wa Ajira.

                                                        

Mpango wa PropelA, unaofadhiliwa na Serikali ya Uswisi na unaolenga kupunguza ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana kwa kuwapatia mafunzo ya stadi zinazohitajika katika soko la ajira, umeanza kutekelezwa katika Kaunti ya Mombasa baada ya kufanikiwa kwa miaka minne katika kaunti ya Nairobi.

Mkuu wa Programu kutoka Swisscontact, Jimmy Delyon, amesema mpango huo unawalenga vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 25, kwa kuwapa mafunzo ya ufundi na uzoefu wa kazi ili kuongeza nafasi zao za kupata ajira na kujiajiri.

                                         

Deylon ameweka wazi kuwa mpango huo kufika kaunti ya Mombasa umekuja wakati ambapo mahitaji ya wafanyakazi wenye ujuzi yanaongezeka katika eneo la Pwani, hasa katika sekta ya ujenzi, huku waajiri wengi wakikabiliwa na uhaba wa mafundi wenye sifa stahiki.

Akiongeza kuwa mpango wa PropelA unalenga kuwapa vijana ujuzi unaohitajika katika soko la ajira, kuongeza nafasi zao za kupata kazi na kuchangia ukuaji wa uchumi kwa kuziba pengo kati ya elimu ya ufundi na mahitaji ya sekta binafsi.

Mkurugenzi mkuu katika kampuni ya Jupiter Energy Solutions Caroline Kanja amesema kampuni hiyo imejitolea kukabiliana na uhaba wa wataalamu wenye ujuzi nchini kupitia ushiriki wake katika mpango wa PropelA, unaolenga kuwapa vijana ujuzi wa kiufundi na kitaaluma unaohitajika katika soko la ajira.

                                     

Kanja amesema kuwa kampuni hiyo imechangia katika kuandaa mtaala wa mafunzo na kudhamini wanafunzi ili kuzalisha wataalamu wenye uwezo wa kuajiriwa au kujiajiri.

Amebainisha kuwa kuajiri wafanyakazi wasio na ujuzi wa kutosha husababisha makosa au uharibifu mkubwa,kurudiwa kwa kazi na kuchelewesha miradi, jambo linaloathiri tija na sifa ya kampuni.

                                      

Akisisitiza kuwa uwekezaji katika mafunzo ya ufundi unawapa vijana ujuzi wa vitendo, kipato cha uhakika na kujiamini, hivyo kuwasaidia kuwa wanajamii wenye tija na wajasiriamali wenye mafanikio.


Comments

Popular posts from this blog

Viongozi wa Kidini PPRL Waunga Mkono Agizo la wizara ya elimu la Ratiba ya Masomo Shuleni

Mbunge Feisal Bader Atuhumiwa Kuzuia Msambweni Talent Show Kufanyika Mvindeni Youth Centre.

Kaunti ya Wajir yaandaa Sherehe za Madaraka Day kwa mara ya kwanza tangu Kenya ipate Uhuru.