Bodaboda 1300 Kaunti ya Mombasa wafaidika na mafunzo na leseni za udereva kuimarisha usalama barabarani.

                                         

Jumla ya wahudum wa bodaboda 1,300 wamenufaika na mafunzo pamoja na kupatiwa leseni za udereva na vyeti vya Recognition of Prior Learning (RPL) katika awamu ya kwanza ya mpango ulioanzishwa na Serikali ya Kaunti ya Mombasa ili kuimarisha usalama barabarani na kurasimisha sekta ya bodaboda.

                                       

Mpango huo ni sehemu ya juhudi za kurasimisha sekta ya bodaboda, ambayo serikali ya kaunti inasema huchangia takriban Shilingi milioni 25 katika uchumi wa Mombasa kila siku, sawa na zaidi ya Shilingi bilioni 9 kwa mwaka.

Akizungumza wakati wa hafla ya kupeana vyeti pamoja na pikipiki,waziri wa barabara na miundombinu katika kaunti ya Mombasa Daniel Manyala, amesema sekta ya bodaboda imekuwa nguzo muhimu ya uchumi wa Mombasa kwa kutoa ajira kwa maelfu ya watu na kusaidia familia nyingi kujipatia kipato.

                                             

Manyala akisema Mombasa ina takriban waendesha bodaboda 30,000, hali inayofanya sekta hiyo kuwa miongoni mwa sekta kubwa zaidi zisizo rasmi katika kaunti hiyo.

Hata hivyo, ameeleza wasiwasi wake kuhusu usalama barabarani, akibainisha kuwa watu 30 walifariki dunia kutokana na ajali za bodaboda mwaka uliopita, wakiwemo waendesha bodaboda 18 na abiria 12. Aidha, watu wengine 220 walijeruhiwa vibaya katika ajali hizo.

                                                  

Kwa mujibu wa serikali ya kaunti, zaidi ya Shilingi milioni 45 zilitumika mwaka jana kugharamia matibabu ya majeruhi wa ajali za bodaboda katika hospitali za umma, huku wengi wao wakipata majeraha makubwa yaliyohitaji matibabu ya muda mrefu.

                                         

Manyala akisema baadhi ya ajali hizo zinasababishwa na ukosefu wa mafunzo stahiki, akifichua kuwa karibu waendesha bodaboda 8,000 bado wanaendesha bila leseni halali za udereva.

Kulingana na Gavana Abdulswamad Shariff Nassir Serikali yake inalenga kuwafikia waendesha bodaboda 3,000 ambao tayari wamewasilisha majina yao kwa ajili ya kushiriki katika mpango huo, huku mafunzo sawia na hayo yakitarajiwa kuwahusisha waendesha pikipiki za usafirishaji wa bidhaa (delivery riders), na pia madereva wa matatu na tuk-tuk.

                                 

Abdulswamad akisema mpango huo unalenga kuboresha usalama barabarani, kuimarisha taaluma katika sekta ya bodaboda na kuongeza fursa za kiuchumi kwa maelfu ya waendesha pikipiki katika Kaunti ya Mombasa.

Comments

Popular posts from this blog

Viongozi wa Kidini PPRL Waunga Mkono Agizo la wizara ya elimu la Ratiba ya Masomo Shuleni

Mbunge Feisal Bader Atuhumiwa Kuzuia Msambweni Talent Show Kufanyika Mvindeni Youth Centre.

Kaunti ya Wajir yaandaa Sherehe za Madaraka Day kwa mara ya kwanza tangu Kenya ipate Uhuru.