Wanafunzi wa Kenya kunufaika na fursa za masomo barani Ulaya.
Wanafunzi wa Kenya wanaotafuta elimu ya juu inayotambulika kimataifa wanatarajiwa kunufaika na fursa mpya baada ya vyuo vikuu vitano nchini kuingia katika makubaliano ya kihistoria na taasisi ya elimu ya juu ya Ulaya, hatua inayofungua njia kwa wanafunzi kutoka kenya kunufaika na kozi mbalimbali.
Chuo Kikuu
cha Danubius International University cha Romania, kwa ushirikiano na kampuni
ya AspiraPath LLC, kimesaini makubaliano na vyuo vikuu vitano vinavyoongoza
nchini Kenya ili kuanzisha mpango rasmi ya kielimu kati ya Kenya na Umoja wa
Ulaya (EU) katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Makubaliano
hayo yalitiwa saini kati ya tarehe 28 Mei na 2 Juni 2026 yanahusisha Amref
International University, Strathmore University, Kabarak University, Moi
University na Pwani University.
Ushirikiano
huo utawezesha wanafunzi wa Kenya kupata nafasi za kusomea shahada za uzamili
(Masters) zilizoidhinishwa na Umoja wa Ulaya kupitia makubaliano ya Erasmus+,
programu za shahada mbili, ushirikiano wa utafiti na mifumo ya kubadilishana
wanafunzi.
Mwanzilishi
wa AspiraPath LLC, Cynthia Kropac, alisema mpango huo unalenga kutoa fursa kwa wanafunzi wa Afrika kutimiza
ndoto zao kupitia fursa za elimu za Ulaya.
Naye Rais na
Mkurugenzi Mtendaji wa Danubius International University, Dr. Steve O. Michael,
alisema ushirikiano huo umejengwa juu ya heshima ya pande zote na dhamira ya
kuboresha maisha ya wanafunzi kupitia elimu bora.
Makamu Mkuu
wa Moi University, Professor Kiplagat Kotut, alisema ushirikiano huo
utaimarisha ubora wa elimu, ubunifu na ubadilishanaji wa maarifa kimataifa.
Kwa upande
wake, Naibu Makamu Mkuu wa Pwani University anayesimamia masuala ya taaluma na
wanafunzi, Professor Hilda Ongayo, amesema ushirikiano wa kimataifa una mchango
mkubwa katika kuimarisha uzoefu wa kujifunza na kuwaandaa wanafunzi kwa
ushindani wa kimataifa.
Makamu Mkuu
wa Kabarak University, Professor Henry Kiplagat, alisisitiza kuwa ushirikiano
huo utafungua fursa zaidi kwa wanafunzi, wahadhiri na watafiti huku ukiimarisha
ubora wa kitaaluma na kitaaluma wa chuo hicho.
Hatua hiyo
inakuja wakati mataifa mengi ya Afrika yanatafuta mbinu mpya za kufadhili elimu
na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ili kuwapa wanafunzi sifa za elimu
zinazotambulika na kushindana katika soko la dunia

Comments
Post a Comment