Mahafala 341 Wahitimu Kozi za utabibu katika Mahafali ya 19 ya chuo cha North Coast Medical Training College.


                                        

Jumla ya mahafala 341 wamefuzu katika vitengo mbalimbali katika taaluma ya utabibu na udaktari katika chuo cha north coast medical training college katika mahafali ya 19.

Akiongea wakati wa hafla hiyo katibu mkuu wa chuo hicho Ruben Waswa amesema chuo hicho kimeendelea kupiga hatua kubwa za maendeleo, kikisajili ongezeko la idadi ya wahitimu kila mwaka kutokana na ubora wa mfumo wake wa elimu na mafunzo.

Ameibainisha kuwa kozi za utabibu zinazotolewa na chuo hicho zinawapa wahitimu fursa kubwa za kupata ajira kwa haraka nchini na katika soko la kimataifa.

                                         

Aidha, amewahimiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao katika vyuo vinavyotambuliwa na kutoa mafunzo bora ili kuwawezesha kupata elimu stahiki, kujiendeleza kitaaluma na kujenga mustakabali wenye mafanikio.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Shule Binafsi nchini (KPSA), Rosebella Ojambo, amesema sekta binafsi ina jukumu muhimu katika kupeana elimu ya matibabu kwa kuziba mapengo yaliyopo katika mfumo wa elimu wa umma.

                                         

Amebainisha kuwa vyuo binafsi vya utabibu vinachangia kupunguza uhaba wa wataalamu wa afya nchini akitoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi ili kuhakikisha elimu bora inawafikia wanafunzi wengi zaidi.

                                       

Nae mmoja wa wakurugenzi wa chuo hicho Marriane Darwinkle Amewapongeza mahafala hao akiwa na Imani kuwa mafunzo na ujuzi waliopata utawawezesha kufanya kazi Kwa weledi sehemu yoyote ulimwenguni na kutoa mchango chanya katika kuboresha huduma za afya na kusaidia jamii                                               


Comments

Popular posts from this blog

Viongozi wa Kidini PPRL Waunga Mkono Agizo la wizara ya elimu la Ratiba ya Masomo Shuleni

Mbunge Feisal Bader Atuhumiwa Kuzuia Msambweni Talent Show Kufanyika Mvindeni Youth Centre.

Kaunti ya Wajir yaandaa Sherehe za Madaraka Day kwa mara ya kwanza tangu Kenya ipate Uhuru.