Ulimwengu Waadhimisha Siku ya Mazingira Himizo la uhifadhi Mazingira likitolewa.

 


Huku ulimwengu ukiadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, wakazi wa Kaunti ya Mombasa wameungana kuadhimisha siku hiyo kwa kushiriki zoezi la upandaji miti katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Afisa Mkuu anayesimamia masuala ya uendelevu wa mazingira katika Kaunti ya Mombasa, Basil Agaga, amesema kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kulinda mazingira huku wakishirikiana kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi licha ya changamoto zinazojitokeza.

Wanamazingira wakipanda miti

Agaga amewahimiza wananchi kukumbatia utamaduni wa kupanda miti ili kusaidia kuhifadhi mazingira na kuboresha hali ya hewa.

Ameahidi kuwa serikali ya kaunti itaendelea kushughulikia changamoto za maji taka na mafuriko ambazo zimekuwa zikiathiri baadhi ya maeneo ya Mombasa.

Kwa upande wake, Michelle Masai kutoka shirika la Midela ameangazia umuhimu wa miti katika kupunguza kiwango cha joto na kuboresha mazingira huku akiwataka wananchi kuacha tabia ya kutupa taka ovyo kwani huchangia uchafuzi wa mazingira na kuziba mifereji ya maji.

                                                

Naye mwanamazingira Zakia Mkanyika ameisihi Serikali ya Kaunti ya Mombasa kuwapa ulinzi akieleza kuwa wamekuwa wakikumbana na changamoto za usalama kutoka kwa baadhi ya wanajamii wanapotekeleza majukumu yao. 

                                          

Vilevile, ameitaka jamii kushiriki kikamilifu katika juhudi za kuhifadhi mazingira, akisisitiza kuwa mazingira safi ni msingi wa afya bora na uhai wa vizazi vya sasa na vijavyo.

Comments

Popular posts from this blog

Viongozi wa Kidini PPRL Waunga Mkono Agizo la wizara ya elimu la Ratiba ya Masomo Shuleni

Mbunge Feisal Bader Atuhumiwa Kuzuia Msambweni Talent Show Kufanyika Mvindeni Youth Centre.

Kaunti ya Wajir yaandaa Sherehe za Madaraka Day kwa mara ya kwanza tangu Kenya ipate Uhuru.