Serikali ya kaunti ya Mombasa kutumia milioni 70 kuboresha Uhuru Gardens.

Serikali ya Kaunti ya Mombasa imetangaza mpango wa kuiboresha Bustani ya Uhuru (Uhuru Gardens) kwa gharama inayokadiriwa kufikia shilingi milioni 70, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha maeneo ya umma na kukuza utalii jijini humo.

Mradi huo unaojulikana kama “Uhuru Gardens 2.0” unalenga kuigeuza bustani hiyo kuwa kituo cha kisasa cha burudani,mwingiliano wa kijamii na kivutio kwa wageni.

Miongoni mwa maboresho yaliyopangwa kufanyika ni pamoja na maeneo ya kupumzika kwa familia, bustani za kuvutia zilizopanuliwa, sehemu ya kisasa ya watoto kuchezea, vifaa vya mazoezi ya nje, pamoja na njia maalum za kutembea na kukimbia Kwa wenye kufanya mazoezi.


Hali ilivyo kwa sasa katika Uhuru Gardens

Mradi huo pia utajumuisha ujenzi wa vyoo vya kisasa na maeneo ya kubadilishia nguo kwa watoto ili kukidhi mahitaji ya familia na wageni wanaotembelea bustani hiyo.

Ili kukuza utamaduni na burudani, bustani hiyo itajengwa ukumbi wa kisasa wa wazi (amphitheatre) kwa ajili ya matamasha ya kitamaduni, shughuli za kijamii na mikusanyiko ya umma.

Aidha, Kituo cha Taarifa za Utalii kitaanzishwa ndani ya bustani hiyo ili kutangaza vivutio vya utalii vya Mombasa na kutoa taarifa kwa watalii wa ndani na wa kimataifa.


Uhuru Gardens kwa sasa 

Maboresho mengine yatakayofanywa ni pamoja na upandaji wa mandhari ya kuvutia, urembo wa mazingira na ujenzi wa ukuta wa usalama kuzunguka bustani hiyo.


watalii wakipiga picha nje ya Uhuru Gardens

Kulingana na wahusika wa kaunti wamesema kuwa baada ya kukamilika, Uhuru Gardens 2.0 itakuwa mojawapo ya bustani bora za umma nchini, ikitoa mazingira salama, ya kisasa na jumuishi kwa watu wa rika zote. 

Comments

Popular posts from this blog

Viongozi wa Kidini PPRL Waunga Mkono Agizo la wizara ya elimu la Ratiba ya Masomo Shuleni

Mbunge Feisal Bader Atuhumiwa Kuzuia Msambweni Talent Show Kufanyika Mvindeni Youth Centre.

Kaunti ya Wajir yaandaa Sherehe za Madaraka Day kwa mara ya kwanza tangu Kenya ipate Uhuru.