Kamati ya Fedha Yaahidi Kujumuisha Maoni ya Wananchi Katika Miswada ya Kifedha.

 


Zoezi la ukusanyaji wa maoni ya wananchi na elimu ya uraia kuhusu miswada mbalimbali ya kifedha limekamilika nchini, huku wananchi wakitoa mapendekezo muhimu yanayolenga kuboresha sera za kodi na usimamizi wa uchumi.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo katika kaunti ya Mombasa, mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango ya Kitaifa Kuria Kimani amesema shughuli hiyo imefanyika katika kaunti 15 zilizoko katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo Wajir, Turkana, Kwale, Kilifi, Tana River, Makueni, Kiambu na Nairobi.

                                                            

Wananchi wakipata fursa ya kujadili Mswada wa Fedha wa mwaka 2026/27, Mswada wa Marekebisho ya Benki Kuu ya Kenya (CBK), Mswada wa Marekebisho ya Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru ya Kenya (KRA) pamoja na Mswada wa Marekebisho ya Hazina ya Taifa ya Uwekezaji (Sovereign Wealth Fund).

Miongoni mwa masuala yaliyoibuliwa ni pendekezo la ushuru wa simu za mkononi. Wananchi wakieeleza kuwa ingawa kuna mpango wa kupunguza kiwango cha ushuru kutoka asilimia 55.5 hadi 50, bado kuna mkanganyiko kuhusu pendekezo la kulipa ushuru wakati wa kuwasha simu kwa mara ya kwanza. Wengi wakipendekeza ushuru huo ulipwe mara moja wakati wa kununua simu.

                                                                 

Aidha, wananchi walitaka wafanyakazi wanaopata mshahara usiozidi Shilingi elfu 30,000 waondolewe ushuru wa PAYE ili kupunguza gharama ya maisha.

Kamati hiyo imeahidi kuwasilisha mapendekezo ya marekebisho ya miswada hiyo bungeni wiki ijayo baada ya kuyajumuisha maoni ya wananchi kote nchini.

Akiongelea swala la safari za Rais nje ya nchi, kiongozi huyo alisema ziara hizo zina manufaa ya moja kwa moja kwa uchumi wa taifa kupitia makubaliano ya biashara na kidiplomasia.

Amesema ziara ya Iran ilifanikisha makubaliano ya kuuza chai ya Kenya moja kwa moja katika soko hilo, huku mazungumzo yaliyofanyika Afrika Kusini yakichangia kuondolewa kwa masharti ya visa kwa Wakenya wanaotembelea nchi hiyo.

                                                              

Akiongeza kuwa hatua hizo zinaimarisha pasipoti ya Kenya na kufungua fursa zaidi za ajira, biashara na utalii kwa wananchi.

Mwenyekiti huyo amesisitiza kuwa mapendekezo yote yaliyokusanywa yatajadiliwa na kuwasilishwa kama marekebisho ya sheria husika.

Pia ameahidi kuwa sauti za wananchi kuhusu ukosefu wa imani kwa viongozi wao zitazingatiwa katika mijadala ya bunge.

                                                            

Amesema watachunguza sababu za kucheleweshwa kwa malipo ya pensheni kwa baadhi ya wastaafu wa Mamlaka ya Bandari Kenya (KPA).

Kamati hiyo ilisema michango ya pensheni hukatwa moja kwa moja kutoka mishahara ya wafanyakazi na kuwekeza, hivyo hakuna sababu ya msingi ya kucheleweshwa kwa malipo baada ya mfanyakazi kustaafu.

Baada ya mchakato wa bajeti kukamilika, kamati hiyo inapanga kuwaita wadau husika ili kutafuta suluhu ya kudumu kwa tatizo hilo ambalo limewaathiri wastaafu wengi wa Mombasa.

Comments

Popular posts from this blog

Viongozi wa Kidini PPRL Waunga Mkono Agizo la wizara ya elimu la Ratiba ya Masomo Shuleni

Mbunge Feisal Bader Atuhumiwa Kuzuia Msambweni Talent Show Kufanyika Mvindeni Youth Centre.

Kaunti ya Wajir yaandaa Sherehe za Madaraka Day kwa mara ya kwanza tangu Kenya ipate Uhuru.